Na Mwandishi Wetu,Kilimanjaro
WASIMAMIZI
wa vyama vya Ushirika Kanda ya kaskazini wamepatiwa mafunzo ya mfumo
mpya wa kieletrokini utakaosaidia kutunza nyaraka na kumbukumbu za
kifedha na mali za ushirika nchini.
Akizungumza wakati akifungua
mafunzo hayo ya siku tatu katika Chuo Kikuu cha Ushirika kwenye ukumbi
wa Pius Msekwa Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, Katibu Tawala mkoa huo
William Machum amesema uhifadhi duni wa nyaraka na kumbukumbu za vyama
kwa baadhi ya vyama kupata hati chafu za ukaguzi .
"Uwazi na
uwajibikaji katika kutunza taarifa za fedha na kutokuwepo na mfumo
thabithi wa ufuatiliaji wa ukaguzi na usimamizi wa vyama ushirika nchini
huchangia kwa kiasi kubwa vyama hivyo kuapta hati chafu na vingine
kufa,"amesema.
Amesema kuwa mfumo huo utasaidia kuboresha kasi ya ukuaji wa vyama vya ushirika na kudhibiti ubadhilifu wa mali za ushirika.
Ameongeza
Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya uanzishwaji na
uendelezaji wa vyama vya ushirika ili kuhakikisha vyama vinakidhi
matakwa na matarajio ya wanachama na kuchangia maendeleo ya Taifa.
Kwa
upande wake Mhasibu Mkuu kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Valency
Karunde amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajenga uwezo maafisa ushirika
kutoka kanda ya kaskazini pamoja warajis wasaidizi wa vyama vya
ushirika wa mikoa hiyo.
Amefafanua kwamba mafunzo hayo pia ni
pamoja usajili wa vyama ushirika kwa njia za kieletrokini ,na kwamba
mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tatu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...