Mkurugenzi Mkuu wa SBL Joe Kariuki  (kulia) akigawa mbolea


Wananchi wakiwa katika foleni kupata mbolea iliyokuwa  akitolewa na kampuni ya SBL

NA MWANDISHI WETU
HATIMAYE Kampuni ys utengenezaji mbolea ya SBL kutoka Kenya imeanza kugawa mbolea bure kwa wakulima wanaofika katika Viwanja vya Kimondo, Mlowo, Mbozi, mkoani Songwe.

Mkurugenzi Mkuu wa SBL Joe Kariuki amesema kwa kila mkulima atakaye fika katika Banda la Kampuni ya Mbolea Tanzania TFC katika maonyesho ya Siku ya Mbolea Duniàni yanayofanyika kitaifa mkoani humo atapata mbolea hiyo bure Kama alivyo ahidi.

Leo wananchi walifurika katika Banda hilo kugombea mbolea hiyo ambayo .

Baahdi ya wananchi hao wameishukuru SBL kwa kugawa bure mbolea hiyo ili kuifanyia majaribio

"Watengenezaji wengi wa mbolea nchini hawatupi wakulima ili tufanye majaribio hivyo mbolea nyingine zinakuwa hazifai SBL wsmefanya vyema kutupa but" amesema Skin Mwakalobo.

Misululu mirefu ili tawala katika Banda la TFC wananchi wakitaka kupata mbolea hiyo inayoelezws kuleta tija kubwa nchini Kenya.

SBL imesema itaendelea kugawa mbolea hiyo bure kwa wakulima nchini kote na ambao watanunua mifuko zaidi ya mitatu watapata mfuko mmoja bure wa mbolea hiyo.

Mbolea hiyo Ina sambazwa na TFC nchini kote na imethibitishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania TFRA ambao ndiyo wandaaji wa maonyesho hayo.

Mbolea hiyo ni organic ambayo imeelezwa kuwa rafiki wa mazingira hivyo kuleta tija katika sekta ya kilimo.

Maonyesho hayo yaliyoanza Jana yatafungwa na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavund

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...