Na.Khadija Seif,Michuzi TV
KLABU
ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)Lugalo
inatarajiwa kusafiri hii leo kwenda Malawi kwaajili ya shindano la siku
Nne Kuwaenzi mashujaa wa Vita ya Pili ya Dunia.
Mkurugenzi
wa Michezo na Utamaduni JWTZ Kanali Martin Msumari amesema,timu ipo
katika maandalizi ya mwisho na wachezaji 12 watakwenda kushiriki
shindano hilo.
Naye
Brigedia Jenerali Joseph Mbilinyi amesema,mpaka sasa timu yao ipovizuri
kwaajili ya shindano na wanatumai wataweza kufanya vizuri kama shindano
walivyofanya katika shindano la Mkuu wa Majeshi “NMB CDF
TROPHY”lilofanyika nchini mwezi uliopita.
Balozi
Mstaafu Job Masima amesema,wao kama wachezaji wamejipanga kikamilifu
kwaajili ya shindano hilo na wanatarajia kwenda kufanya vizuri na kurudi
na ushindi nyumbani.
Wachezaji
12 Wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara na
Meja Jenerali Ibrahim Mhona na Mwenyekiti wa Lugalo Brigedia Jenerali
Mstaafu Michael Luwongo ni miongoni mwa Wachezaji hao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...