WAANDISHI
wa habari wameomba kushirikishwa kila hatua yanayofanyika katika
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ili kupata uwanda mpana
wakuwajuza wananchi kuhusu mambo mbalimbali katika Jumuiya hiyo.
Wito
huo umetolewa na wandishi wa habari wa vyombo tofauti waliposhiriki
semina ya kuwajengea uwezo kuhusu Jumuiya hiyo iliyoandaliwa na Mtandao
wa wakulima wa Afrika Mashariki na nchi za Kusini mwa Afrika (ESAFF)
kwa kushirikiana na Kituo cha Malengo ya Maendeleo Endelevu Afrika
(SDGCA).
Semina hizo ni
moja ya utekelezaji wa Mradi wa Mpango Jumuishi wa Kujenga Uwezo wa
Kitaasisi (IICB) kwa Sekretarieti ya SADC na Wadau wa Kitaifa kwa
kushirikiana na wadau wake katika kufikia ahadi za kikanda hususan,
Mpango Elekezi wa Kikanda wa Maendeleo (RISDP) - (2020-2030) na Dira ya
2050 ya SADC.
Kati ya
waliotoa maoni namtazamo juu ya Jumuiya hiyo ni Mwenyekiti wa Taasisi ya
Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) Salome Kitomari ambapo
alisema katika kuhabarisha huko kwa sasa kinachofanywa ni waandishi
kutakiwa wakati kunapokuwa na matukio kama vile ujio wa viongozi na
mikutano mbalimbali mikubwa inayofanyika.
Amesema
hii ni tofauti na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao wamekuwa wepesi
katika kutoa taarifa na kufungua milango ya kupata taarifa muda wowowte
wanapohitajika.
“Kutokana
na hilo waaandishi wanajikuta wanafunga kwa kuripoti tukio la mkutano
,au kusubiri taarifa kutoka wizarani au Ikulu kuhusu yanayojiri katika
Jumuiya hiyo jambo ambalo halina afya katika taaluma ya habari licha ya
kuwa kuna mambo mengi yakuandika kuhusu Jumuiya hiyo kikiwemo
changamoto, mafanikio na fursa mbalimbali zilizopo kwa nchi wanachama.
Kwa
upande wake Tausi Mbowe kutoka kituo cha redio Times, amesema
kumekuwepo na utoaji wa tuzo za waandishi wanaoandika habari za SADC,
lakini ni kama kwa upande wa Tanzanaia zinawabagua kwa kuwa wengine
huandika kwa lugha ya Kiswahili.
Amesema
ifike mahali kwa kuwa Kiswahili kimechaguliwa kuwa lughha ya
kuzungumzwa na umoja huo,basi katika shughuli zake zote lugha hii ipewe
kipaumbe.
“Tunaandika
sana Makala zinzohusu SADC, lakini zikifika kwa majaji inaelezwa
zimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili, hii sio sawa na kama ni katika
kuwaridhisha wafadhili wa tuzo hizo basi vema kukawe kwa majaji wanaojua
lugha hii ili iwe rahisi kuzipitia zinazotoka Tanzania,”,alisema
Tausi.
Aidha kwa upande
wake Dorcus Raymond kutoka Channel Ten, alisema bado kuna ukitirimba
katika kupata taarifa kwa wadau mbalimbali waandishi wanapotaka
kukamilisha habari zao.
Zaah alipendekeza kuwepo
kwa klabu za SADC kuanzia shule nakwenye mashirikisho ya sekta
mbalimbali yatayakosaidia kushua elimu na taarifa ya Jumuia hiyo.
Philipo
Mhava kutoka redio Clouds,amesema hata lugha ya Kiswahili imekuwa ngumu
kutumika katika utoaji taarifa unazohusu Jumuiya hiyo na kuwatenga hata
watanzania wakawaida kuifahamu na kufuatilia yanayoendelea ndani ya
Jumuiya hiyo.
Kwa upande
wake Mratibu wa ESAFF, Joe Mzinga,amesema malengo ni kuhakikisha vyombo
vya habari vinajengewa uwezo na kuwezeshwa kuweza kutoa habari zaidi
kuhusu SADC, aliongeza kua kuna haja ya kushirikisha vyombo vya habari
katika ngazi zote, tafsiri ya taarifa mbalimbali ili kuakisi muktadha wa
ndani, kutoa mafunzo kwa vyombo vya habari kuhusu jinsi ya kusambaza
taarifa, kuandaa utaratibu wa ushiriki wa kimkakati wa AZAKi-Vyombo vya
Habari, makala ya video ya baadhi ya mafanikio kuhusu ushirikiano wa
kikanda wa SADC.
Mzinga
ameeleza kuna makundi mbalimbali yanapaswa kushirikishwa katika Jumuiya
hiyo ikiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali, madhebu ya dini na taasisi
zingine na hakuna anayepaswa kuchwa nyuma.
Akizungumza
kwenye washa hiyo, Ambrose Rwaheru kutoka SDGC amesema shirika lake
litaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu mtangamano wa
SADC.
Mradi huo umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya na unatekelezwa katika nchi za Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe,
Mwandishi wahabari Dorcus
Raymond kutoka Channel Ten, alisema bado kuna ukitirimba katika kupata
taarifa kwa wadau mbalimbali waandishi wanapotaka kukamilisha habari zao
Ambrose Rwaheru kutoka SDGC amesema shirika shirika lake litaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu mtangamano wa SADC.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...