KAMPUNI ya ulinzi ya kibinafsi ya SGA Security imeshinda tuzo ya mwajiri bora miongoni mwa makampuni ya ulinzi yanayofanya kazi Zanzibar.

Tuzo hiyo imetolewa na Waziri wa Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mhe. Mudriki Soraga, katika hafla iliyoandaliwa kwa pamoja na chama kikuu cha wafanyakazi Zanzibar (ZAFICOWU) na Chama cha Waajiri Zanzinbar (ZANEMA).

Waziri Soraga aliipongeza SGA kwa kuonyesha kwa kuwa mfano bora kwa makampuni na taasisi zingine, ambapo alisema ushindi wa SGA unadhihirisha wazi ya kuwa inawezekana kufuata kikamilifu sheria za kazi na bado mtu au taasisi zikapta mafanikio katika biashara.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa ZAFICOWU, Saraphina Maasare, ameipongeza kampuni ya SGA kwa kupata tuzo hiyo.

“Huwa tunapata ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa uongozi wa SGA, ambapo pamoja na mambo mengine huwa tunashirikiana na kushauriana na uongozi wa SGA ikiwemo ule unaohitajika kabla ya mfanyakazi kuchuliwa hatua za kinidhamu”, alisema.

"Kiwango cha ushirikiano ni cha kupongezwa na hii inaonesha sababu za wateja wengi kuichagua kampuni ya SGA kama mtoa huduma wao”, Bi Maasare aliongeza.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa SGA, Bi. Mosumba Wambura, alifafanua kuwa SGA ina miongozo inayoeleweka kuhusu ushirikishwaji wa wafanyakazi, vyama vya wafanyakazi na Serikali, ambayo alisema ni muhimu haswa linapokuja swala la kushauriana katika ngazi zote ili kuhakikisha kwamba wafanyakazi wanapata haki zao ili kuepuka migogoro kazini.

"Siri yetu ni kuendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wote muhimu ambao ni pamoja na vyama vya wafanyakazi na Serikali kwa ujumla”, alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa SGA Tanzania Bw Eric Sambu, aliwapongeza mameneja wake wa ngazi ya kati kwa kutekeleza ahadi zinazotolewa na uongozi wa kampuni hiyo ambapo alisema ni pamoja na kuainisha shughuli na matakwa ya Serikali ya Zanzibar yanayohusiana na jinsi ya kufanya biashara.

Alisema kuwa SGA inajivunia kuwa mwajiri bora, mkubwa zaidi na mwenye rekodi ya wafanyakazi wa muda mrefu, ambapo alisema miongoni mwao ni wale ambao wana Zaidi ya miaka 20 kazini jambo ambali alisema linaashiria ushirikiano mzuri ulioko kati ya uongozi na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

"Tunaamini katika kufuata masharti ya leseni yetu inayotaka kufanya kazi kwa mujibu way ale yote tunayowaahidi wadau wote”, alisema.

SGA ndiyo kampuni kongwe zaidi ya ulinzi nchini Tanzania ambapo kwa sasa ina zaidi ya wafanyakazi 6,000.

SGA inatoa huduma za ulinzi, mahitaji ya dharura ya wateja, usimamizi na usafirishaji wa pesa taslimu, mahitaji yote yanayohusiana na maswala ya usalama ikiwemo kupitia huduma za kielektroniki na huduma za usafirishaji wa vifurushi.

Kampuni ina vyeti vinne vya ubora unaotambuliwa na taasisi ya viwango ya kimataifa ya ISO, ambapo ilichaguliwa kupitia kura za wateja kama kama mtoaji huduma za usalama anayependelewa zaidi na aliye na vifaa vya kisasa katika Ukanda wa Afrika Mashariki katika Tuzo za Chaguo la Wateja Afrika kwa mwaka wa 2022.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Sekta ya Usalama Tanzania (TSIA), Felix Kagisa, aliwapongeza waandaaji wa hafla hiyo kwa kutambua waajiri wanaotekeleza majukumu yao vyema.

Alielezea kutokuridhishwa kwake na vita ya malipo kwa ajili ya huduma miongoni mwa makampuni, jambo ambalo baadhi ya wakurugenzi wa makampuni waliohudhuria pia walisema ni tatizo kubwa kwa kuwa hakuna bei elekezi inayohusiana na huduma zinazotolewa na kampuni binafsi za ulinzi.

"Bei za chini zinazotozwa na baadhi ya makampuni si endelevu, na hivyo kufanya kuwa vigumu kuzingatia matakwa ya sheria za kazi", Bw Kagisa aliongeza.

Alitoa wito kwa makampuni mengine kuiga kampuni ya SGA ambayo alisema imeonesha mfano mzuri na wa kuigwa katika kutekeleza majukumu yake ambapo alisema ndiyo njia sahihi ya kufanya biashara.


Waziri wa Kazi, Uchumi na Uwezeshaji Zanzibar,Mh. Mudriki Soraga akikabidhi tuzo ya mwajiri Bora miongoni mwa makampuni ya ulinzi Zanzibar kwa mwakilishi wa SGA Security, Bi Mosumba Wambura katika hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...