Bus la abiria la kampuni ya AL- SAEDY lenye namba za usajili T995 DLB likiwa limepinduka katika barabara kuu ya Morogoro - Dar es salaam eneo la Kitungwa Manispaa ya Morogoro

Bus la abiria la kampuni ya AL- SAEDY baada ya kuinuliwa


 


Na Jackson Jaspaly wa Michuzi TV, Morogoro


Bus la abiria la kampuni ya AL- SAEDY lenye namba za usajili T995 DLB limepinduka Katika barabara kuu ya Morogoro - Dar es salaam eneo la Kitungwa Manispaa ya Morogoro baada ya kutaka kukwepa kugongana uso kwa uso na bus la ALLY’S STAR lenye namba za usajili T 947 EBF lililokuwa likitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Mwanza na kusababisha majeruhi mmoja, na wengine 57 wamenusurika kifo waliokuwa katika bus ya AL – SAEDY..

 

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro FORTUNATUS MUSILIMU amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa bus aina ya DRAGON la kampuni ya ALLY’S STAR lenye namba za usajili T 947 EBF lililokuwa likitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Mwanza na kuovateki bila ya kuchukua tahadhali na kutaka kugongana uso kwa uso na bus la AL – SAEDY, lililokuwa likitokea Mkoani Morogoro.

 

WAZUNGUMZAJI.

 

FORTUNATUS MUSILIMU, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro.

 

EMANUEL OCHIENG, Kamanda msaidizi wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Morogoro.

 

ALLY JUMA, Shuhuda wa ajali.

MWISHO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...