-Pia yakabidhi mitungi ya gesi 700 na majiko yake bure kwa
wananchi, viongozi
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
IKIWA
ni sehemu ya dhamira yake ya kielimu na sera yake ya Mazingira, Kijamii
na Utawala “ESG”, Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Ltd, “OGTL”, imeamua
kutoa mafunzo ya nishati ya gesi safi ya kupikia kwa viongozi wa wilaya
zote za mkoa wa Kilimanjaro lengo likiwa kujenga ufahamu kuhusu LPG,
matumizi yake salama na jinsi kupika kwa kutumia LPG.
Sambamba na
mafunzo hayo ambayo yanalenga kuboresha afya ya jamii huku kukilinda
mazingira, Oryx pia imekabidhi mitungi ya gesi pamoja na majiko yake kwa
viongozi wa ngazi mbalimbali katika kata zote za mkoa wa Kilimanjari na
hayo yamefanyika kwa ushirikiano kati ya OGTL na Mbunge wa Viti Maaklum
Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond.
Akizungumza wakati wa
mafunzo hayo yaliyoshirikisha washiriki 700 ambao ni wawakiishi wa
wananchi kutoka katika wilaya zote saba za Mkoa wa Kilimanjaro,
Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Araman Benoite amesema LPG inaweza kuwa
hatari ikitumiwa au kutumiwa vibaya. Hata hivyo, ikitumiwa kwa uangalifu
na kiwango kinachofaa cha mafunzo na maarifa, Oryx LPG ndiyo nishati
safi inayofaa kutumika kwa kupikia.
Ndiyo maana OGTL imeunda miongozo hii ya mafunzo kuhusu matumizi salama ya LPG.
“Matumizi
ya LPG yanaendelea nchini Tanzania. Ni wajibu wa wadau wa LPG
kuhakikisha Wateja wa LPG wanaelimishwa na kufunzwa kwa njia ambayo
wanafahamu kuhusu manufaa yote mazuri ya LPG na jinsi ya kuitumia kwa
usalama. Ndio maana Oryx Gas Tanzania imeamua kuzindua mafunzo haya ya
usalama kwa watumiaji wake pamoja na elimu ya msingi kuhusu suluhisho la
kupikia safi la Oryx LPG.
“Hakuna kitu muhimu zaidi kuliko
usalama wa wateja wa OGTL. Hivyo mafunzo ya aina hii yamekuwa kipaumbele
sambamba na ukuzaji wa suluhu za Oryx Gas LPG nchini Tanzania. Mafunzo
ya aina hii yatatekelezwa hatua kwa hatua kwa jamii zote nchi zima na
kwa muda mrefu Oryx Gas Tanzania imeendesha mafunzo kwa makundi
mbalimbali ya watumiaji kama vile Super Dealers, Dealers, Retailers.
“
OGTL pia imeungana na wadau wakuu kama vile EWURA, Vikosi vya Zimamoto,
Wakala wa Uzito na Vipimo ambao wamesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza
uelewa kuhusu usalama wa LPG kwa wauzaji na wasambazaji. Sasa kampuni ya
Oryx Gas Tanzania imeamua kwenda kwenye ngazi ya watumiaji wamwisho,
jambo ambalo tunaamini ni jambo sahihi kuelimisha wateja kwa matumizi
salama ya LPG huku tukipunguza hatari ya ajali kutokea kwa kukosa
maarifa,”amesema Benoite Pamoja na hayo amesema mbali na kutoa mafunzo,
vibandiko (Stickers) vya usalama vya LPG hubandikwa kwenye mitungi yote
ya Oryx Gas ili kuwakumbusha watumiaji wote kuhusu misingi ya usalama wa
LPG.
Akizungumzia majukumu muhimu Benoite amesema wahusika wakuu
katika tasnia ya LPG - yaani wazalishaji, wasambazaji, wafanyabiashara,
watengenezaji vifaa, na wasafirishaji na hata mafundi -wana majukumu
makubwa katika kukuza usalama.“ Sisi sote kama wadau tushirikiane chini
ya bendera ya Tanzania LPG Association ili kuhakikisha utekelezaji mzuri
wa mpango wa matumizi salama wa LPG,kuendeleza mazoea mazuri na kupiga
vita vitendo viovu.
“Mamlaka za kitaifa na za mitaa zinafaa
kuchukua fursa ya utaalamu ndani ya sekta ya LPG ili kuhakikisha mbinu
za pamoja za utendaji mzuri wa usalama. Wateja wanapaswa kufuata maagizo
ya usalama ambayo hutolewa kwao. Kuna wadau wengine wengi, na wote wana
jukumu muhimu la kutekeleza.Viongozi na wananchi wataruhusiwa kueneza
elimu waliyoipata ufahamu vyema zaidi katika idadi ya watu wa Tanzania.”
Awali
Katibu Mkuu wizara ya Nishati Mhandisi Felichesmi Mramba amesema Wizara
hiyo inaendelea na mikakati kuhakikisha watanzania wengi wanatumia
nishati safi ya kupikia ya gesi na kwa sasa wanaendelea kuzungumza na
wabunifu na kampuni kubwa kuangalia uwezekano wa gesi iwe inanunuliwa
kama unavyonunuliwa umeme.
Amesema nishati ya kupikia inagusa
kila mtu na haiepukiki hivyo ni vema Wizara ya Nishati ikawa na mikakati
inayowezesha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia.“Watanzania
wengine wamekuwa wamekuwa wakitumia nishati ambayo ina madhara kwa afya
na mazingira.”
Aidha amesema nia ni kuona nchi inahama kutoka
kwenye nishati chafu ya kupikia na kwenda kwenye nishati safi ya
kupikia.Hata hivyo gharama ya kutumia mkaa kwa mwezi mmoja kwa familia
ya watu watano ni kubwa zaidi kuliko kutumia mtungi wa gesi.
“Wizara
tunafikiria kukutana na wabunifu pamoja na kampuni kubwa za gasi kwa
ajili ya kuangaliauwezekano wa gesi iwe inanunuliwa kama vile
unavyonunua umeme kwa Luku kupitia simu ya mkononi na hiyo itasaidia
kuwezesha wananchi kumudu gharama kulingana na kipato. Tunataka ifike
wakri mtu akiwa na Sh.1000 anaweza kununua gesi na akapika , au akiwa na
Sh.10,000 basi anunue gesi.” Kwa upande wake Mbunge Shally Raymond
amemshukukuru Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania
Araman Benoite
kwa kutoa mafunzo hayo mkoani Kilimanjaro sambamba na kutoa mitungi ya
gesi na majiko yake bure kwa viongozi wa kata zote za mkoa wa
Kilimanjaro huku akisisitiza kuwa Kilimanjaro imeamua kutoka kwenye
nishati chafu ya kupikia na kutumia nishati safi ya kupikia ya gesi.Mkurugenzi
wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Araman Benoite akitoa maelekezo ya
namna ya kuwasha moto kwenye jiko la mtungi wa gesi ya Oryx kwa
washiriki wa mafunzo ya usalama kuhusu nishati ya gesi ya kupikia
yaliyofanyika kwa washiriki 700 kutoka kwenye Wilaya zote saba za mkoa
waKilimanjaro.Mafunzo hayo yameandaliwa na Oryx Gas kwa kushirikiana na
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kilimanjaro Shelly Raymond. Mbali ya
mafunzo pia kampuni hiyo imekabidhi mitungi 700 na majiko yake kwa
viongozi hao wa kata pamoja na wananchi.
Mkurugenzi
wa Oryx Gas Tanzania Araman Benoite akizungumza wakati wa mafunzo
yaliyolenga kutoa elimu kuhusu usalama wa gesi na tabia zake kwa
washiriki 700 ambao wanatoka katika kata zote za mkoa wa Kilimanjaro
ambapo lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha jamii inakuwa salama
nakuepukana na madhara yanayoweza kutokea iwapo mtungi wa gesi utatumika
vibaya.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo hayo wakielekezana namna ya kuwasha moto kwenye
mtungi wa gesi ya Oryx huku Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Araman
Benoite(aliyesimama katikati) akiwa makini kufuatilia.
Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felichesmi Mramba (wa kwanza kulia)
akiwa makini kumsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Araman
Benoite (wa pili kushoto) kabla ya kuanza kwa mafunzo ya usalama na
kuelewa tabia za gesi kwa yaliyotolewa kwa washiriki 700 katika Mkoa wa
Kilimanjaro.
Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond akizungumza wakati wa
mafunzo kuhusu usalama wa nishati ya gesi ya kupikia yaliyoandaliwa na
Kampuni ya Oryx Gas Tanzania na mbunge huyo.Jumla ya washriki 700 kutoka
kwenye kata zote za mkoa wa Kilimanjaro wameshirikimafunzo hayo
sambamba na kupewa mitungi ya gesi ya Oryx pamoja na majiko yake.
Sehemu
ya washiriki wa mafunzo yaliyohusu usalama wa nishati ya gesi ya
kupikia majumbaniwakifuatilia maelezo mbalimbali yaliyokuwa yanatolewa
na Meneja Masoko wa Oryx Gas Tanzania PeterNdomba(hayuko pichani)
alipokuwa akielezea hatua kwa hatua namna ya kutumia mtungi wa gesi
yaOryx.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felichesmi Mramba akizungumza wakati akifungua
mafunzo
hayo yaliyofanyika Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro huku akitumia nafasi
hiyo kuelezea hatua ambazo zinachukuliwa na Wizara hiyo katika
kutekeleza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu kuelekea kwenye
matumizi ya nishati safi ya kupikia.Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya usalama na uelewa wa tabia za gesi
wakiondoka kwenye mafunzohayo wakiwa na mitungi ya Gas ya Oryx ambayo
wamepewa bure pamoja na majiko yake lengo likiwa kuhamasisha nishati
safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa inayoharibu
mazingira na afya.
10:Mmoja wa maofisa wa Oryx Gas Tanzania akimtwisha mtungi wa gesi mmoja ya washriki wa mafunzo
hayo.Washiriki wa mafunzo hayo wakiweka vizuri mitungi yao baada ya kukabidhiwa na kampuni ya Oryx
Gas TanzaniaMeneja
Masoko wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Peter Ndomba akimtishwa mtungi
wa gesi mmoja ya wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro baada ya kukabidhiwa
mtungi huo pamona na jiko lake.Oryx wametoa mitungi 700 pamoja na majiko
yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...