Benki ya Exim tawi la Mwanza imekabidhi msaada wa majaketi yenye viakisi mwanga (Reflector Jackets) kwa madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wa mkoani humo ikiwa ni sehemu ya jitihada ya benki hiyo katika kukabiliana na ajali za barabarani zinazotokea mkoani humo hususani nyakati za usiku.
Hafla ya makabiodhiano ya majaketi hayo ilifanyika kwenye tawi la benki hiyo mkoani humo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo maofisa wa benki hiyo wakiongozwa na Meneja wa Benki hiyo tawi la Mwanza Bw Edwin Polle, Meneja Mahusiano wa benki hiyo mkoa wa Mwanza Bi Sarah Tito, wawakilishi kutoka jeshi la Polisi, kikosi cha Usalama Barabarani wakiongozwa na Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Mwanza, ASP. Sunday Ibrahim pamoja na wawakilishi wa madereva wa pikipiki mkoa huo.Meneja wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Mwanza Bw Edwin Polle (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa majaketi yenye viakisi mwanga (Reflector Jacket) kwa mmoja wa viongozi wa madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wa mkoani humo Bw. Ally Abdulmajid ikiwa ni sehemu ya jitihada ya benki hiyo katika kukabiliana na ajali za barabarani mwishoni mwa mwaka. Anaeshuhudia ni Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Mwanza, ASP. Sunday Ibrahim. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye tawi la benki hiyo mkoani Mwanza jana.
Meneja wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Mwanza Bw Edwin Polle (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa majaketi yenye viakisi mwanga (Reflector Jackets) kwa Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Mwanza, ASP. Sunday Ibrahim kwa ajili ya madereva wa pikipiki wa mkoa huo ikiwa ni sehemu ya jitihada ya benki hiyo katika kukabiliana na ajali za barabarani mwishoni mwa mwaka. Wanaoshuhudia ni pamoja na Meneja Mahusiano wa benki hiyo mkoa wa Mwanza Bi. Sarah Tito. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye tawi la benki hiyo mkoani Mwanza jana.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Mwanza, ASP. Sunday Ibrahim (katikati) akikabidhi sehemu ya msaada wa majaketi yenye viakisi mwanga (Reflector Jackets) kwa ajili ya madereva wa pikipiki wa mkoa huo yaliyotolewa na Benki ya Exim tawi la Mwanza ikiwa ni sehemu ya jitihada ya benki hiyo katika kukabiliana na ajali za barabarani mwishoni mwa mwaka. Wanaoshuhudia ni pamoja Meneja wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Mwanza Bw Edwin Polle (kushoto). Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye tawi la benki hiyo mkoani Mwanza jana.
Baadhi ya madereva wa bodaboda waliowakilisha madereva wa mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya majaketi ya kuakisi mwanga (Reflector Jackets) yaliyotolewa na benki ya Exim tawi la Mwanza ikiwa ni sehemu ya jitihada ya benki hiyo katika kukabiliana na ajali za barabarani mwishoni mwa mwaka. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye tawi la benki hiyo mkoani Mwanza jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...