Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) hii leo imeorodhesha hati fungani yake ya kwanza kabisa ya NBC Twiga katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Hati fungani hiyo ya muda wa kati ya TZS 300 bilioni, ilifunguliwa katika soko la awali tarehe 31 Oktoba 2022, na hivi karibuni benki hiyo ilitangaza kufunga mauzo ya hati fungani hiyo kwa mafanikio makubwa baada ya kukusanya kiasi cha sh Bil 38.9 ikilinganishwa na sh bil 30 zilizotarajiwa kukusanywa hapo awali. Mafanikio hayo ni asilimia 130 ya malengo yaliyotarajiwa..
Kupitia hati fungani hiyo, Benki hiyo inalenga kukusanya kiasi cha Sh 300 Bilioni ambazo zitatumika katika kufadhili sekta ndogo na za kati, Kilimo na sekta nyinginezo muhimu kiuchumi nchini.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kuorodhesha hati fungani hiyo kwenye soko la Hisa la Dar es Salaam iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa wa Wizara ya Fedha na Mipango,Japhet Justine aliipongeza Benki ya NBC kwa hatua hiyo kwa kuwa itafungua zaidi soko la hisa huku pia akibainisha kuwa upatokanaji wa fedha hizo hizo utasaidia zaidi jamii ya wafanyabiashara nchini.
‘Mbali na kuunga mkono msukumo wa ujumuishi wa kifedha kupitia hati fungani hii, serikali inafurahishwa zaidi kujua kwamba faida za hati funganii hii inakwenda mbali zaidi kwa kugusa mnyororo mzima wa wadau wa kilimo na wajasariamali. Serikali inapongeza benki ya NBC kwa ubunifu huu,’’ alisema
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, Mkurugenzi wa Hazina wa Benki ya NBC, Peter Nalitolera, alisema mafanikio makubwa ambayo benki hiyo imeyapata kupitia hati fungani hiyo ni ishara kwamba wananchi wanaendelea kuiamini zaidi benki hiyo huku akiipongeza serikali kwa kuandaa mazingira wezeshi yaliyochagiza mafanikio hayo.
‘Leo, tuna furaha kuorodhesha Twiga Bond katika soko la DSE ili kuruhusu biashara zaidi kwa umma. Sasa wawekezaji walionunua hati fungani wakati wa soko la msingi wanaweza kufanya biashara kwa urahisi, wakati wale ambao hawakufanikiwa hapo awali wanaweza kununua kupitia madalali wa soko la hisa,” alisema
Akitoa mchanganuo kuhusu aina ya wawekezaji wa hati fungani hiyo Bw Nalitolera alisema: ‘Tulikuwa na maombi 639, kati ya hayo asilimia 97 walikuwa wawekezaji reja reja, na ni asilimia 3 tu ndio walikuwa wanunuzi kutoka mashirika. Hii ni ishara tosha ya kuimarika kwa juhudi katika elimu ya masuala ya fedha katika nchi yetu, ambapo sasa Watanzania wengi wanaelewa umuhimu wa kuwekeza kwenye hati fungani na dhamana za fedha. Rekodi zetu zinaonyesha kuwa wanawake walichangia 42% ya wawekezaji wote wa rejareja (241). Hili ni hatua kubwa katika juhudi zetu za ushirikishwaji wa kifedha.’’
Awali akizungumza kwenye hafla hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Bi Mary Mniwasa aliipongeza benki ya NBC kwa hatua hiyo muhimu huku akibainisha kuwa ushiriki wa benki hiyo katika soko hilo unaifanya DSE kufunga mwaka huu kwa kuorodhesha kwa hati fungani mbili za kampuni binafsi.
“Hati fungani mbili zilizoorodheshwa ndani ya mwaka huu zinafanya idadi ya hati fungani za kampuni ambazo zimeorodheshwa DSE kufikia tano zenye thamani ya jumla ya Tsh bilioni 186.67. Kiasi hicho kinaweza kuonekana kidogo, lakini kinaonyesha jitihada kubwa zinazofanyika’’. alisema.
Akizungumza katika hafla hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw.Nicodemus Mkama, pamoja na kuipongeza benki ya NBC kwa mafanikio hayo, pia aliipongeza serikali kwa kuweka mazingira wezeshi ambayo yamewavutia wawekezaji wengi zaidi kwenye hati fungani hiyo.
"Mafanikio hayo yamesababishwa kwa kiasi kikubwa na mazingira wezeshi ya serikali, hasa hatua yake ya kuondoa ushuru wa zuio kwenye hati fungani za makampuni, hatua ambayo imevutia wawekezaji zaidi kwenye hati fungani za mashirika binafsi,’’ alibainisha.
Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa wa Wizara ya Fedha na Mipango,Japhet Justine (katikati) akigonga kengele kuashiria kuorodheshwa rasmi kwa hati fungani ya NBC Twiga katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) wakati wa hafla fupi ya uorodheshwji huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Pamoja naye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Bi Mary Mniwasa (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Hazina wa Benki ya NBC, Peter Nalitolera (kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw. Nicodemus Mkama (wa pili kulia) na mwakilishi wa Bodi ya benki hiyo Bw . Felix Mlaki (kulia)
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kuorodhesha hati fungani hiyo kwenye soko la Hisa la Dar es Salaam iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa wa Wizara ya Fedha na Mipango,Japhet Justine (pichani) aliipongeza Benki ya NBC kwa hatua hiyo kwa kuwa itafungua zaidi soko la hisa huku pia akibainisha kuwa upatokanaji wa fedha hizo hizo utasaidia zaidi jamii ya wafanyabiashara nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bw.Nicodemus Mkama (pichani) pamoja na kuipongeza benki ya NBC kwa mafanikio hayo, pia aliipongeza serikali kwa kuweka mazingira wezeshi ambayo yamewavutia wawekezaji wengi zaidi kwenye hati fungani hiyo.
Awali akizungumza kwenye hafla hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Bi Mary Mniwasa (pichani) aliipongeza benki ya NBC kwa hatua hiyo muhimu huku akibainisha kuwa ushiriki wa benki hiyo katika soko hilo unaifanya DSE kufunga mwaka huu kwa kuorodhesha kwa hati fungani mbili za kampuni binafsi.
Mwakilishi wa Bodi ya wakurugenzi benki ya NBC Bw Felix Mlaki (pichani) akizungumza kwenye hafla hiyo aliahidi kuisimamia vyema benki hiyo kuhakikisha kwamba fedha hizo zinatumika kulingana na malengo ya hati fungani hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, Mkurugenzi wa Hazina wa Benki ya NBC, Peter Nalitolera (pichani), alisema mafanikio makubwa ambayo benki hiyo imeyapata kupitia hati fungani hiyo ni ishara kwamba wananchi wanaendelea kuiamini zaidi benki hiyo huku akiipongeza serikali kwa kuandaa mazingira wezeshi yaliyochagiza mafanikio hayo.
Meneja Miradi Soko la Hisa Dar es Salaam Bw Emmanuel Nyalali akizungumza kwenye hafla hiyo.
Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa wa Wizara ya Fedha na Mipango,Japhet Justine (katikati walioketi) sambamba na viongozi waandami wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) pamoja na wafanyakazi wa Benki ya NBC wakati wa hafla fupi ya uorodheshwaji wa hati fungani ya NBC ijulikanayo kama NBC Twiga Bond huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa wa Wizara ya Fedha na Mipango,Japhet Justine (katikati walioketi) sambamba na viongozi waandami wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Benki ya NBC wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa DSE wakati wa hafla fupi ya uorodheshwaji wa hati fungani ya NBC ijulikanayo kama NBC Twiga Bond iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hafla hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...