Benki ya NMB imekabidhi vifaa
vya kusaidia maendeleo ya elimu wilayani Kibaha vyenye thamani ya zaidi
ya TZS milioni 37 kama sehemu ya kuchangia ustawi wa huduma za kijamii
nchini.
Kiasi hicho ni sehemu ya asilimia moja ya faida baada ya
kodi ambayo benki hiyo utenga kila mwaka kusaidia kutatua changamoto
zinazoikabili jamii na kuwekezakatika miradi ya maendeleo.
Akizungumza
kabla ya makabidhiano hayo, Meneja waTawi la NMB Kibaha, Bw Festo
Isango, aliyemwakilisha Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam inayojumuisha
piaMkoa wa Pwani, alisema bajeti ya mwaka huu ya benki hiyo ya
uwajibikaji kwa jamii ni zaidi ya TZS bilioni mbili.
“Kwa miaka
kadhaa sasa, NMB imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ya
wananchi kwa kujikita zaidi kwenye miradi ya elimu (madawati na vifaa
vya kuezeka), afya (vitanda, magodoro yake na vifaa vingine vya kusaidia
matibabu) na kusaidia majanga yanayoipata nchi yetu,” Bw Isango
alibainisha.
“Na kwa zaidi ya miaka saba mfululizo tumekuwa
tukitenga asilimia moja ya faida yetu kama sehemu ya uwajibikaji kwa
jamii inayotuzunguka,” akiongezea.
Hafla ya kukabidhi vifaa
hivyo kwa ajili ya shule nne za sekondari na mbili za msingi ilifanyika
kwenye ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Bi Sara Msafiri, aliyeipongeza
benki hiyo kwa ushiriki wake wa dhati katika maendeleo taifa.
Kwa
mujibu wa Bw. Isango, kiwango cha uwekezaji cha NMB katika miradi ya
maendeleo ni kikubwa sana kinachoifanya benki hiyo kuwa kinara wa ustawi
wa jamii miongoni mwa taasisi za fedha nchini na vifaa waliyokabidhi
leo ni moja ya ushiriki wao katika maendeleo ya jamii.
Shule
zilizopata msaada wa benki hiyo jana ni shule za msingi Sofu na
Mwanabwito. Za sekondari ni Mwanalugali, Pangani, Kibaha Girls na Mbawa
Miswe. Usaidizi zilizoupata ni wa samani za ofisi za walimu, meza na
viti vya wanafunzi, vitanda, makabati pamoja na mabati.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha mkoani
Pwani, Sara Msafiri, akiangalia kabati za kuhifadhia vitabuzilizotolewa
kwa Shule ya Msingi Sofu sh. Milioni 37 iliyofanyika katika viwanja vya
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB
Tawi la Kibaha, Festo Issango
Mkuu
wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Sara Msafiri, akiangalia Viti 50 na
meza vilitolewa katika hafla ya makabidhiano ya misaada mbalimbali
kutoka NMB kwa shule sita wenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 37
kwaShule ya Sekondari Pangani wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa
shule za Sekondari na msingi za wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...