Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Mshambuliaji wa Ufaransa, Karim Mostafa Benzema rasmi ametangaza kustaafu kucheza soka la Kimataifa ikiwa ni siku moja, baada ya taifa hilo kukosa ubingwa wa Michuano ya Kombe la Dunia 2022 mbele ya Argentina.

Benzema aliondolewa kwenye kambi ya timu hiyo ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kindumbwe ndumbwe cha Michuano hiyo iliyohitimishwa nchini Qatar, Benzema aliondolewa kwenye Kikosi cha Ufaransa kutokana na majeruhi, huku wengine wakidai kuwa alikuwa hana mawasiliano mazuri na Uongozi wa timu.

“Nilifanya jitihada na makosa, yaliniweka hapa nilipo leo, najivunia kwa hilo, nimeandika historia na huu ni mwisho”, ameandika Karim Benzema kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Benzema anastaafu kucheza soka la Kimataifa akiwa tayari amecheza michezo 97 na amefunga mabao 37 tangu aanze kucheza timu hiyo ya Ufaransa mwaka 2007.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...