Njombe
MWENYEKITI wa halmashauri ya Mji wa Njombe Erasto Mpete pamoja na mkurugenzi wa halmashauri hiyo wamefanikiwa kukabidhi mradi wa vyumba vya madarasa kwa mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa mara baada ya kukamilika kwa 100% mradi ambao ni wa vyumba 26 iliyopatiwa milioni 520 kutoka Serikali kuu.
Akizungumza Kwa niaba ya madiwani na halmashauri hiyo Mwenyekiti Mpete amesema
"Kwa niaba ya halmashauri ya mji wa Njombe tunatoa shukrani kwa Mh Rais kwa kutupatia fedha Mil 520 kwa madarasa haya 26 kwasababu naamini tusingofika hapa na leo hii tumekamilisha na kuyakabidhi kwa mkuu wetu wa wilaya"Amesema Erasto Mpete
Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ameipongeza halmashauri kwa kujenga madarasa kwa viwango huku wakikamilisha kwa wakati.
"Nimeridhika na ujenzi wa madarasa uliofanywa na halmashauri ya mji wa Njombe,ujenzi umekamilika kwa wakati na yamejengwa kwa viwango,sasa jukumu letu lililobaki ni kuhakikisha watoto wanakuja shuleni wanasoma na kufaulu"amesema Kissa Kasongwa
Kasongwa ameongeza kuwa miongoni mwa jambo kubwa la kuishukuru serikali ni pamoja na ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Mabatini ambapo palikuwa na madarasa yaliyojengwa muda mrefu.
"Hapa Mabatini Sekondari kulikuwa Kuna madarasa yaliyojengwa mwaka 1954 yalikuwa tu yanakarabatiwa lakini wakati huu wa Rais Dkt,Samia yamebomolewa na kujengwa mengine Kwa viwango"
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...