HATUA ya kwanza, ni kuchoronga na kujenga njia ya kuchepusha maji ya mto ili ili kupata eneo kavu katikati ya mto ili kuweza kujenga tuta kubwa litakalohifadhi maji.
Hatua ya pili, ni kujenga tuta kuu la kuhifadhi maji.
Hatua ya tatu, ni kuchoronga na kujenga njia za kuporomosha maji ili yaweze kuzungusha vinu vya kufua umeme.
Hatua ya nne ni kujenga, kuunga na kusimika mitambo na vinu vya kufua umeme.
Hatua ya tano ni kujenga kituo cha kusafirisha umeme ili uweze kutumika katika gridi ya taifa.
Hatua ya sita ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka bwawa la Nyerere mpaka Chalinze ili kuingiza umeme kwenye gridi ya Taifa na kutumiwa na wananchi.
Hatua ya saba ni ujenzi wa daraja la kudumu.
Hatua ya nane ni ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa mradi na barabara za ndani ya mradi.
#BwawaLetuLaNyerere #HatuaKubwaYaKihistoria #KuelekeaUmemeWaUhakika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...