Na Jane Edward, Arusha


Wakazi wa jiji la Arusha na Tanzania kwa Ujumla wametakiwa kuchangamkia huduma za kibingwa zinazotolewa na madaktari bingwa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka ndani na nje ya nchi kwa kupima afya zao na kupata tiba ikiwemo magonjwa ya saratani.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuona zoezi la upimaji wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha ,Dk Silvia Mamkwe amesema huduma inayotolewa na madaktari bingwa kutoka hospitali ya kimataifa ya Apollo iliyopo nchini India kwa kushirikiana na hospitali ya Saint Joseph iliyopo jijini Arusha ni ya muhimu sana.

Dk Mamkwe amesema, kumekuwepo na ushirikiano mzuri kati ya madaktari bingwa kutoka nje ya nchi wanaokuja nchini kutoa huduma za matibabu kwa lengo la kuwapunguzia gharama wananchi kufuata matibabu nje ya nchi ,hivyo amewataka kuwa mstari wa mbele kuchangamkia fursa hiyo na kuweza kutibiwa.

"Hapo awali tulikuwa tukikakabiliwa na changamoto ya vifaa vya uchunguzi "city scan " katika hospitali nyingi za rufaa hali iliyokuwa ikiwalazimu wananchi wengi kufuata huduma hiyo nje ya nchi ila kwa sasa hivi vifaa hivyo vipo vya kutosha ,hivyo nawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupata huduma."amesema Dk Mamkwe.

Aidha amesema kuwa, takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 30 ya wananchi mkoani Arusha wanasumbuliwa na matatizo ya magonjwa yasiyoambukiza ,hivyo elimu zaidi inahitajika kutolewa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kuweza kupatiwa matibabu ya haraka.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Saint Joseph ,Thobias Mkina amesema kuwa,idadi ya magonjwa yasiyoambukiza yamezidi kuongezeka siku hadi siku hivyo uwepo wa madaktari bingwa kutoka nchini India kunasaidia sana wananchi kuweza kupata huduma hiyo kwa haraka na kuokoa gharama ya kufuata huduma hiyo nje ya nchi.

Dk Mkina amesema kuwa, wamekuwa na ushirikiano wa karibu na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Apollo ambapo wameweka kambi siku mbili kwa ajili ya kutoa huduma ya magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya saratani ya kizazi, matiti,koo,utumbo,Kansa ya damu, ngozi,ini,kibofu cha mkojo na tezi dume na magonjwa ya Figo.

"ujio wa madaktari hawa bingwa kutoka nchini India kunatoa fursa pia kwa madaktari wetu kuweza kujifunza zaidi kupitia wao na madaktari wetu watatoka hapa na kwenda nchini India kwa lengo la kujifunza zaidi kutoka kwao na kambi hizi zitakuwa zikifanyika kila baada ya miezi mitatu ambapo kwa awamu hii ya kwanza tunatarajia kuwafikia zaidi ya wananchi 3,000 "amesema Dk Mkina.

Kwa upande wake ,Afisa masoko kutoka hospitali ya Apollo nchini India ,Vuran Sukhija amesema kuwa,matarajio yao ni kuona wananchi wa Arusha wanahudumiwa na kupatiwa huduma nzuri za matibabu kutoka kwa madaktari bingwa wawili kutoka hospitali hiyo ya Apollo.

Nao Baadhi ya wagonjwa walionufaika na huduma hiyo ,Mery Kasian kutoka jijini Dar es Salaam na Irene Matemu wameshukuru kwa ujio huo huku wakiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuwepo kwa kambi za mara kwa mara kutoka kwa madaktari bingwa pamoja na kuomba huduma hiyo iwe endelevu hapa nchini hususani Mkoa wa Arusha kwani wananchi wenye uhitaji ni wengi.

Afisa masoko kutoka  hospitali ya Apollo  nchini India ,Vuran Sukhija akielezea umuhimu wa zoezi la upimaji nchini.
Dr Silvia Mamkwe Mganga Mkuu wa Mkoa akizungumza na wadau wa hospital ya St Joseph jijini Arusha.
Dr Silvia Mamkwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa hospital ya ST Joseph Thobias Mkina akifafanua lengo la zoezi la upimaji kwa waandishi wa habari.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...