Na Janeth Raphael,Michuzi TV

RAIS aliyerejeahwa madarakani baada ya kuwa nje takribani miezi 13 wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Leah Ulaya amesema moja ya mipango yake ni kuhakikisha anarejesha umoja na mshikamano ndani ya Chama hicho na kuondoa makundi mingoni mwa wanachama wa chama na kwenye safu ya uongozi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 16, 2022 baada ya kupitishwa kuwa Rais wa Chama hicho… amesema unapokuwa unamiliki kundi kubwa kama hilo la walimu lazima kuwepo na makundi, lakini makundi hayo ni lazima yawe yote yanalenga mlengo mmoja, yasiwe yanayoelekea kugawanya Chama.

“Kwa hiyo mimi kama Kiongozi Mkuu lakini kiongozi mzoefu sitarajii kuendekeza makundi yaliyokuwa yamejengeka kwa kiasi fulani.Ninasema hivyo kwasababu nimekuwa ndani ya Chama cha Walimu Tanzania lakini hata nilipokuwa nje, kwa kipindi hicho makundi yalijidhirisha wazi na kwa maana hiyo sasa kama kiongozi mkuu nakemea kusiwe na makundi.

“Nitajitahidi kwa kushirikiana na viongozi wenzangu kuhakikisha tunakomesha kabisa makundi yanayotugawana hatimaye tunakosa nguvu ya kufanya vile ambavyo wanachama wanatarajia, ”amesema ...

Akieleza makundi wakati wa uchaguzi amesema katika chaguzi wowote hata iwe Mwenyekiti wa mtaa au balozi lazima kuwepo na watu wanaotamani mtu wao ashinde lakini baada ya uchaguzi lazima kuungana na kufanya kazi ile ambayo kundi kuhusika wanahitaji.

“Kwa hiyo katika utaratibu wa makundi ni namna na silka ya kiongozi anayeingia anavyohitaji makundi lakini moja ya vitu ambavyo nimekuwa nikipiga vita ni kuwa na makundi. Kwa sasa makundi hayo natarajia hayatakuwepo.

“Kama yalikuwepo wakati mimi sipo basi kwa kuwa nimerudi nitafanya kila namna kukaa na viongozi na makundi mbalimbali ili kuhakikisha tunayavunja makundi na kufanya kazi ambayo walimu wanaihitaji..."

Aidha ametumia nafasi hiyo kuahidi yuko imara na ataendelea kusimamia kanuni na katiba lakini kazi yao kubwa ni kutetea maslahi ya wanachama ambao ni walimu wote wa Tanzania.

"Kwa utaratibu ambao tunao kama chama tutaendelea kudumisha umoja na mshikamano , kufanikisha yale ambayo wanachama wanatarajia."

 

Rais wa chama cha walimu Tanzania  (CWT) Mwalimu Leah Ulaya akizungumza Mara baaada ya wajumbe wa Mkutano mkuu wa chama hicho kumrejesha madarakani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...