-Wanahabari kuwa sehemu ya kuelimisha kuhusu uharibifu wa mazingira


Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv

Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika Kongamano la Kujadili kukauka Mto Ruaha litakalofanyika Desemba 19 mkoani Iringa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari, Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA) Habib Mchange amesema kuwa kongamano hilo linalenga kujadili kukauka mto Ruaha ikiwa wanahabari ni sehemu ya kuhakikisha wanatumia karamu ya kuelimisha madhara ya wananchi kufanya shughuli za kibinadamu.

Mchange amesema mabadiliko ya Tabianchi ni mabadiliko ya Tabia za wanadamu hivyo wanahabari ni nguzo katika kuhakikisha masuala ya mazingira linasimamiwa pamoja sheria ziheshimiwe.

Amesema mito inayoingiza maji kwenye bonde la Usangu inatiririsha maji wakati wote lakini mto Ruaha haina maji kabisa.

Amesema kuwa mara ya kwanza Mto Ruaha ulikauka 1994 ambapo serikali ilichukua hatua ukatiririka kwa muda tena ukakauka 2005 hadi sasa unakauka ambapo sasa ni wakati wa waandishi kuchukua karamu.

Aidha amesema kuwa kongamano hilo litaaziamia nini kifanyike katika kufanya mto Ruaha irudi kwenye kutiririsha maji

Mto Ruaha ndio inayochangia umeme kwa asilimia 15 kwenye bwawa la Mtera na tegemeo kwa bwawa la nyerere hivyo mgao wa umeme watu hawajui.

Amesema mgao wa umeme ulipoanza ni matokeo ya mto Ruaha kukauka ambapo miradi ya umeme ndio ikaanza ikiwemo mradi wa IPTL 2005 ukaanza.

Kwa upande wa Ofisa Mawasiliano wa MECIRA, Hamisi Mkotya,amesema kuwa wanahabari wana wajibu wa kupaza sauti kusemea jambo hilo kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika mambo mengine ili kupambana na uharibifu huo wa mazingira na vyanzo vya maji.

“Unapoharibu mazingira au vyanzo vya maji, haumkomoi mtu, unajikomoa wewe mwenyewe. Kuna shughuli za binadamu zinafanyika kiholea au isivyo halali na kuharibu mazingira na vyanzo vya maji. Kuna kilimo kinafanyika kiholela, ufugaji wa kuingiza mifugo katika maeneo ambayo hayaruhusiwi, kwa hiyo yote hayo, rasilimali zinavyoharibika, taifa linapata hasara, lakini tunaathirika sisi sote",amesema Mkotya .

Nae Mjumbe wa MECIRA na Mdau mkubwa wa mambo ya Uhifadhi nchini,Mwandishi mkongwe wa Habari, Manyerere Jackton amebainisha kuwa wajibu wa wanahabari ni kujipambanua badala ya kuwa sehemu ya watu wanaolalamika, kutumia kalamu zao kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira hayo.

“Mazingira yanapo athirika hayachagui mtu, sisi wote tunaathirika. Leo hii kuna mgawo wa umeme, watu wote wanaathirika bila kujali itikadi ya mtu, kwa hiyo tumeona sisi kama wanahabari tulete mabadiliko chanya katika suala hili la kutunza na kuhifadhi mazingira yetu kwa sababu tunao wajibu huo wa kushirikiana na serikali kuelimisha jamii,”alisema Manyerere.


Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari ,Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA) Habib Mchange akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) leo Desemba 11,2022 jijini Dar es Salaam kuhusu kufanyika kwa kongamano kubwa litakalohusisha Wahariri na Wanahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya Digitali, Blog, Redio, Televisheni, na Magazeti; Mawaziri, Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Mashirika ya umma, Mashirika ya kimataifa, na Wadau mbalimbali wa uhifadhi na utunzaji wa mazingira kujadili na kutafuta suluhu ya hali inayoendelea ya uharibifu wa mazingira nchini, litakalofanyika katika ukumbi wa Chuo kikuu cha Mkwawa mkoani Iringa,ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR (MICHUZI MEDIA).

Mjumbe wa MECIRA na Mdau mkubwa wa mambo ya Uhifadhi nchini,Mwandishi mkongwe wa Habari, Manyerere Jackton akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kwa Waandishi wa Habari ikiwemo kuwakumbusha wajibu wao wa kujipambanua badala ya kuwa sehemu ya watu wanaolalamika, kutumia kalamu zao kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira hayo.

 Ofisa Mawasiliano wa MECIRA, Hamisi Mkotya akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) akiwaomba Wanahabari kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha wanapaza sauti na kusemea jambo hilo la uharibifu mkubwa wa mazingira kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika mambo mengine ili kupambana na uharibifu huo wa mazingira na vyanzo vya maji.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...