-Ataka nguvu kubwa iwekwe kuwaunga mkono Rais Dk. Samia, Dk. Mwinyi
-Makamu wa Pili wa Rais Adullah awakata upepo wasaka vyeo, wapiga majungu
Na MWANDISHI WETU, Zanzibar
KATIBU
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu
Shaka amewataka wana CCM kutopoteza muda kwa malumbano na majibizano
kwa kuwa kuna kazi muhimu mbele yao ya kujenga Chama na nchi.
Amesema
Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi wameanza vizuri uongozi katika
kuwatumikia wananchi, hivyo ni jukumu la wana CCM na Watanzania kwa
jumla kuwaunga mkono.
Aidha,
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah amewataka
wale wenye tamaa ya kutaka vyeo kujitafakari na kuchapa kazi kwa kuwa
kazi kubwa Sasa ni kuijenga nchi.
Shaka
aliyasema hayo jana katika mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Zanzibar) Dk. Hussein Ali Mwinyi yaliyofanyika katika viwanja vya Afisi
Kuu ya CCM Zanzibar (Kisiwandui) na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
"Niwaombe
wana CCM wenzangu tusipoteze muda wa marumbano, tuna kazi ya kukijenga
Chama tuna kazi ya kuijenga nchi, tuna kazi ya kuijenga Zanzibar hii.
Dk. Mwinyi ameanza vizuri jasiri mwongoza njia lazima wafuasi
tufuate...bega kwa bega," alisema.
Shaka
alisema Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kipo katika mikono salama chini ya
uongozi wa Dk. Mwinyi kwa kuwa ameonyesha uwezo mkubwa wa uongozi na
kusimamia maendeleo ya wananchi.
"Makamu
Mwenyekiti umekabidhiwa jahazi hili hatuna wasiwasi na wewe,
umekabidhiwa jahazi hili likiwa salama 'inshallah' (Mungu akipenda)
utatuvusha...wewe ni nahodha jabari, wewe ni nahodha makini utatuvusha.
Wasiojua waanze kupata salamu tunakuja na Dk. Mwinyi," alisema.
Katibu Mwenezi Shaka alisema moja ya mambo ambayo CCM haijawahi kukosea ni katika kuwapata viongozi makini wa kuivusha nchi.
Shaka
alisema kasi ya Rais Dk. Mwinyi imeanza kuwatisha baadhi ya watu
waliokuwa na tamaa ya madaraka ambao sasa wameanza kutapatapa.
"Nimesikia kwamba wanafikiria sijui watasusa, msuse msisuse shughuli ipo," alisema.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali
Mwinyi akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kuelekea katika hafla
ya mapokezi yake iliyofanyika Afisi Kuu ya Makao Makuu ya CCM Zanzibar
(Kisiwandui). (Picha zote na Fahad Siraj wa CCM).
Wananchi mbalimbali wakimpungia Mkono Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi. (Picha na Fahad Siraj wa CCM).
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais
Dk. Hussein Ali Mwinyi, akiwapungia mkono wananchi wakati wa mapokezi
yake baada ya kuchaguliwa kuwa mkmu Mwenyekiti wa CCM. Hafla ya mapokezi
ilifanyika jana kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid
Karume, hadi Afisi Kuu ya Makao Makuu ya CCM Zanzibar (Kisiwandui).
(Picha zote na Fahad Siraj wa CCM).
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar
Mstaafu, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akimkaribisha
Dk. Hussein Ali Mwinyi, akimkaribisha Mkamu Mwenyekiti wa mpya wa CCM,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali
Mwinyi wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika Afisi Kuu ya Makao Makuu ya
CCM Zanzibar (Kisiwandui). (Picha na Fahad Siraj wa CCM).
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi
akizungumza katika hafla ya mapokezi yake baada ya kuchaguliwa kushika
wadhifa huo wiki iliyopita jijini Dodoma, hafla ya mapokezi hayo
ilifanyika Afisi Kuu ya Makao Makuu ya CCM Zanzibar (Kisiwandui).(Picha na Fahad Siraj wa CCM).
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)
ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza wakati wa
mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi baada ya
kuchaguliwa kushika wadhifa huo wiki iliyopita jijini Dodoma, hafla ya
mapokezi hayo ilifanyika jana Afisi Kuu ya Makao Makuu ya CCM Zanzibar
(Kisiwandui). (Picha na Fahad Siraj wa CCM).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...