Na Oscar Assenga,TANGA
Mbunge wa Jimbo la Mkinga Dastan Kitandula amemuomba Waziri Mkuu Kasim Majaliwa kulichukua suala la makundi yaTembo kuvamia mashamba ya Mkonge na kuharibu mazao lipatiwe ufumbuzi kutokana na kwamba linawarudisha nyuma juhudi za wakulima wadogo ikiwemo kuwakatisha tamaa.
Amesema pamoja na Serikali kuweka msukumo kwa wakulima wadogo kujiingiza kwenye kulima zao hilo kinyume na ilivyokuwa zamani lakini kutokana na uwepo wa changamoto hiyo unawashusha hari wakulima.
Kitandula aliyasema hayo wakati akitoa salamu zake wakati wa Mkutano wa tatu wa wadau wa Sekta ya Mkonge Tanzania iliyofanyika Jijini Tanga iliyokwenda sambamba na kauli mbiu ya Mkonge ni Biashara Wekeza Sasa ambapo Waziri Mkuu aliwakilishwa na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde.
Alisema licha ya kufurahishwa na jinsi Serikali inavyojielekeza kufufua zao la Mkonge na jitihada zinazofanyika na msukumo unaowekwa kwa wakulima wadogo wajiingize kwenye kulima zao hilo tofauti na ilivyokuwa siku za kinyume na hadi kuonekana kuwa zao wakulima wakubwa ambapo kwasasa mwako umekuwa mkubwa hasa kwa wakulima wadogo.
"Lakini lipo jambo ambalo Serikali inabidi ilichukulie kwa umuhimu mkubwa ili lisiwakatishe tamaa wakulima wa zao hilo hasa changamoto ya makundi ya Tembo kuvamia mashamba ya Mkonge"Alisema
"Hii ni changamoto kubwa sana na tumejitahidi kusema serikalini bado ni changamoto hivyo tunaomba mh Waziri Mkuu ulichukue ukazungumze na wenzako kwamba muone namna kudhibiti Tembo ili wasituulie zao la Mkonge pamoa na mengine" Alisema Mbunge Kitandula.
Hata hivyo Mbunge huyo alisema tamaa yao vilevile ni kuona wakati jitihada za kufufua zao wajielekeze kwenye maeneo mengine wataongeza thamani ya zao hilo ili kutengeza fedha ili Utafiti ifanyike tuweze kupata mafanikio zaidi kwenye zao hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...