Na Andrew Chale,Dar es Salaam.

Kampuni ya ONASTORIE imewezesha Wabunifu wa Kitanzania wakiwemo Wanafunzi wa Vyuo mbali mbali Nchini kushiriki kwa mara ya kwanza shindano la dukuzi za Kibunifu kwenye upande wa Teknolojia ya Uhalisia ongezi.

OnaStories wameendesha mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika ukumbi wa Dlab Kijitonyama Dar es Salaam kwa kushirikiana na Wadau kampuni ya META (zamani Facebook),IMISIED,Dlab na Blackrhino ambapo mwisho washindi walizawadiwa zawadi ikiwemo fedha za kusaidia bunifu zao.

Awali akizungumza katika mafunzo hayo, Mshirika mwenza wa kampuni hiyo,Bi. Tulanana Bohela alisema kuwa, mafunzo hayo ni kwa mara Kwanza yanafanyika nchini yakisimamiwa na OnaStories huku yakifanyika pia nchi zingine 16,

ambapo washindi wa jumla watakutana pamoja kwa Bara la Afrika katika mafunzo makubwa zaidi hapo baadae.

"Tanzania ikiwa ni miongoni mwa Nchi 16 Barani Afrika ikiwa ni zaidi ya washiriki 1,000, OnaStories ikiwa ndio muendeshaji mkazi wa Udukuzi huo hapa nchini, ikiweza kupata makundi kumi yaliyoshiriki kikamilifu ndani ya siku hizo tatu za kutafuta (kudukua) wazo tatuzi na lenye manufaa katika jamii ya Kitanzania". Alisema Tulanana Bohela

Na kumalizia kuwa, mawazo hayo yalijikita kwenye sekta ya elimu, afya, utalii, Biashara na ubunifu ambapo Udukuzi huo ukiwa ni muendelezo wa hatua ya awali ya Pre-Hackathon ambapo washiriki walikutanishwa na wataalamu kutoka pande zote za Afrika na kufundishwa mbinu mbalimbali na njia bora ya kutumia na kutengeneza wazo kupitia teknolojia za Uhalisia ongezi." Alisema Tulanana Bohela.

Washindi katika shindano hilo, kundi la kwanza walizawadiwa dola 1,500 Usd na kupata nafasi kwenye mashindano makubwa zaidi ya Bootcamp yanayoanza January hadi mwezi April, ambapo itakaribisha nchi 16 za Afrika.

Aidha, washindi wengine wakiwemo Washindi wa pili walizawadiwa dola 800 huku mshindi wa tatu dola 700.

Aidha, washiriki washindi wa Kwanza kutoka hapa nchini watashiriki Mashindano ya Afrika yanayofahamika kama Bootcamp ambapo mshindi wa kwanza wa nchi zote 16 zitakazoshiriki na huko watapita miezi mitatu ya mafunzo, maboresho ya mawazo yao na ushindani.

"Hii Bootcamp itakua Januari hadi April, Mshindi wa kwanza atapatiwa dola 10,000, wa pili dola 8,000 na watatu atapatiwa dola 7,000.


 Kiongozi mwenza wa kampuni ya OnaStories Bi. Tulanana Bohela (katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na washiriki hao.
Viongozi wenza wa kampuni ya OnaStories Bi. Tulanana Bohela (kushoto) na Bw.Princely Glorious (katikati) akitangaza washindi wa kwanza wa shindano hilo.
Viongozi wenza wa kampuni ya OnaStories Bi. Tulanana Bohela (wa Kwanza kushoto) pamoja na wa Pili kulia Bw.Princely Glorious wakiwa pamoja na washindi, wakikabidhi mfano wa hundi ya zawadi kwa kundi bora la kwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...