Njombe
Mwili wa aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Ruvu Shooting FC, Graham Enock Naftari (Gira) umepumzishwa kwa heshima ya kijeshi mkoani Njombe mara baada ya kufikishwa nyumbani kwao katika kata ya Kidegembye iliopo Lupembe halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Uongozi wa timu ya Ruvu Shooting,Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF pamoja na Jeshi la kujenga Taifa ambao ndio walikuwa waajili wake wamefanikiwa kuusafirisha mwili wa mchezaji GIRA kutoka jijini Dar es Salaam Mpaka mkoani humo huku Msemaji wa Clabu ya Ruvu Shooting Masau Bwile akibainisha kuwa kifo cha mchezaji huyo imekuwa ni pigo kubwa kwao.
“Lengo letu ilikuwa wanapomaliza kozi warejee kuungana na wachezaji wenzao kwa ajili ya kutumika kwenye timu yetu na tulitarajia tunapoanza mzunguko wa pili timu yetu itakuwa na nguvu mpya kwa kuwapata hawa wachezaji walioondoka mwanzoni mwa msimu akiwemo yeye ili kuja kutusogeza mbele na pengine kututoa kwenye nafasi ambayo tupo kwa sasa kutokana na upungufu wa wachezaji hawa waliokwenda mafunzo ya kijeshi”amesema Masu Bwile
Mwakilishi kutoka shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) Ndug.Abousufian Sillia amesema kifo cha mchezaji huyo ni pigo kubwa kwani kwasasa Taifa linahitaji wachezaji wenye umri mdogo ambao wanajituma kama ilivyo kuwa kwa mchezaji huyo wakati wa uhai wake
Marehem Graham Naftari alifariki Disember 1,2022 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu huku akiwa na umri wa miaka 23.
Home
Unlabelled
Mchezaji wa Ruvu Shooting azikwa kwa heshima Njombe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...