Na Farida Mangube, Morogoro
WATU watatu wamefariki dunia baada ya Gari aina ya Land Cruiser, mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kugongana na Lori la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kisha kupoteza muelekeo na kuwagonga watu hao waliokuwa pembeni karibu na ajali hiyo.

Akizungumza na Michuzi Blog, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Morogoro, Fotunatus Musilim amesema ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Decemba 5, 2022 katika eneo la Kihonda Barabara kuu ya Morogoro – Dodoma.

Kamanda Musilim amewataja waliofariki kuwa ni Ashirafu Yusuph (43) Dereva wa Pikipiki yenye usajili namba MC 367 DFM Kampuni ya Houjue na Abiria wake, Faustine Polinali (28) wote wakazi wa Kihonda Manispaa ya Morogoro na Robison Mazengo( 25) mkazi wa Mkundi aliyekuwa akiendesha Pikipiki yenye namba za uasajili 450 DDL, Houjue.

Kamanda huyo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva Abed Namangae (53) mkazi wa Mkundi Manispaa ya Morogoro aliyekuwa akiendesha gari namba T514 CAQ Toyota Land Cruzer mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, amesema wakati akitokea eneo la Mkundi kuelekea mjini alilipita gari la JWTZ lenye namba za usajili 2032JW12 Ashock Land Cruzer.

Aidha, Kamanda Musilim amesema baada ya kuligonga Gari hilo na kupoteza uelekeo aliwagonga watu hao waliokuwa kwenye Pikipiki na kusababisha vifo vyao.

Kamanda amesema Dereva huyo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro anashikiliwa na Jeshi la Polisi na atafikishwa Mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Kwa upande wake Afisa Habari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Scholastica Ndunga amethibitisha kupokea miili ya watu wawili na majeruhi mmoja ambaye naye alifariki muda mfupi wakati akipatiwa anapatiwa matibabu hospitali hapo.

"Ni kweli tumepokea miili ya watu wawili na majeruhi mmoja ambaye alifika hapa akiwa katika hali mbaya na baada ya muda mfupi naye akafariki dunia," amesema Scholastica.

Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mkude amesema mmoja wa marehemu hao ni Dereva wa Daladala na alipanda Bodaboda kwa ajili ya kuwahi kuchukua Daladala yake alilokuwa amelaza kwenye kituo cha Mafuta Kihonda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...