Mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo akitoa amaelekezo ya kujaza fomu ya kujiunga na NSSF kwa mwanachama wa UWAMAGATE jijini Dar es Salaam leo.

MHADHIRI Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo amewaomba taasisi sinazotoa huduma za hifadhi za jamii kutoa elimu kwa wananchi na wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi juu ya huduma na fursa walizonazo.

Ametoa rai hiyo leo Desemba 31, 2022 wakati alipokuta na Wanachama wa Umoja wa Madereva na Makondakta wa Daladala za Gerezani Tegeta jijini Dar es Salaam 
(UWAMAGATE),walipokutana katika mkutano Mkuu wa Mwisho na wa kufunga mwaka ikiwa ni kutaka kupanga mipango ya mwaka ujao na kuangalia ni wapi wametekeleza na wapi hawajatekeleza. Pia amewaasa Viongozi wa Vyama hivyo kushirikiana ili kutoa elimu kwa wanachama wake.

Dkt. Kinyondo amewaasa wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi kama Wajasiliamali wadogo, Wafanyakazi wa Sekta za Ujenzi na wafanyakazi wa Sekta ya Usafirishaji kuwekeza katika Mifuko ya hifadhi za jamii kwani watapata faida baadae ambapo watakuwa hawanauwezo wa kufanya kazi tena kama sasa.

"Sisi Mzumbe tumefurahia kuona Wafanayakazi wa Sekta zisizo rasmi wameanza kujiunga na Mifuko ya hifadhi za jamii kama NSSF ambapo kujiunga na mifuko hiyo kwa kuchangia kiasi cha shilingi 20,000/= kwa kila mwezi kutawasaidia hapo baadae." Amesema

Amesema kuwa wanaona fahari kuona Matokeo ya Utafitiwalioufanya kuanzia 2017 hadi kusambaza matokeo yake kwa wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi wameanza kujiunga na mifuko hiyo ingawa baadhi yao hawana taarifa za kutosha kutoka kwa taasisi zinazotoa huduma za hifadhi za jamii.

Dkt. Kinyondo amesema kuwa Viongozi wa Mifuko ya hifadhi za jamii wanatakiwa kushirikiana na Viongozi wa Vikundi pamoja na Viongozi wa serikali za mtaa ili kutoa elimu kwa wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi kwaajili ya kuwaelimsha wanachama kujiunga na mifuko hiyo ili waweze kujiunga. Amesema wanachama wanapo pata taatifa wanaonesha nia ya kujiunga lakini amesisitiza taarifa zitolewe kwa wahusika.

"Wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi wanahitaji taarifa na fursa zilizopo katika taasisi zinazotoa huduma za hifadhi za jamii kama NSSF, CHF, Bima za Afya na UTTwahusika watoe taarifa katika maeneo ya Stendi za Daladala, vijiwe vya bodaboda pamoja na maeneo ambayo wafanyakazi hao wanafanya shughuli zao." Amesema Dkt. Kinyondo

Kwa Upande wa Mtafiti Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Aloyce Gervas amesema kuwa Mfuko wa hifadhi za jamii wa NSSF wameweza kuandikisha wanachama zaidi ya 50 kutoka chama cha Waendesha daladala za Gerezani Tegeta. Amesema matokeo chanya yameanza kuonekana kupitia utafiti walioufanya.

Pia amewaomba wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi kuendelea kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii kwani utafiti ulionesha kuwa ni asilimia chache ndio wamejiunga na mifuko hiyo pamoja na kuomba mikopo kwenye taasisi za Fedha.

Kwa upande wa Mjumbe wa kamati Tendaji wa UWAMAGATE, Ramadhani Simba amewapongeza Watafiti chuo kikuu Mzumbe kwa kutoa elimu. "Wametusaidia mpaka sasa tumeshaanza kujaza fomu za kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii pamoja na kukata bima za afya, hii ni fursa adhimu kwetu wana UWAMAGATE. "

Pia amewaomba wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi kujiunga katika vikundi ili waweze kupata fursa za mafunzo pamoja na kupata elimu ya mifuko ya hifafhi za jamii pamoja na bima za afya, kupitia vikundi gharama zinapungua na wanapata faida kubwa zaidi.
Mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 31, 2022 wakati alipokuta na Wanachama wa Umoja wa Madereva na Makondakta wa Daladala za Gerezani Tegeta jijini Dar es Salaam.
Mtafiti Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Aloyce Gervas akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 31, 2022 wakati alipokuta na Wanachama wa Umoja wa Madereva na Makondakta wa Daladala za Gerezani Tegeta jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa kamati Tendaji wa UWAMAGATE, Ramadhani Simba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 31, 2022.
Mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo akizungumza na wanachama wa UWAMAGATE, jijini Dar es Salaam leo.Mtafiti Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Aloyce Gervas akizungumza na Wanachama wa Umoja wa Madereva na Makondakta wa Daladala za Gerezani Tegeta jijini Dar es Salaam (UWAMAGATE), leo Desemba 31, 2022.
Afisa Maelekezo NSSF Sekta isiyorasmi, Joseph Bayo akitoa elimu kwa wanachama wa UUMAGATE jijini Dar es Salaam leo.

Picha ya pamoja.

Baadhi ya wanachama wa UWAMAGATE wakiwa katika mkutano mkuu wa Chama chao jijini Dar es Salaam leo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...