Na.Khadija Seif -, Michuzi TV
SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) wamesema watahakikishia wanaendelea kuweka Mazingira mazuri kwa wasanii wa Filamu katika maafa na hasara itakapotokea wakati wa kutengeneza kazi zao za sanaa.
Akizungumza na Wasanii pamoja na wadau wa Filamu nchini Leo Disemba 16,2022 Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Mkoani Kilimanjaro John Mdenye wakati akizungumza kwenye Semina fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Ngurudoto Jijini Arusha amesema shirika lao linahuduma mbalimbali ambapo kwa wasanii watanufaika nazo ikiwemo huduma ya bima ya Ajali.
"Tunafahamu changamoto wanazopitia wasanii wanapokua kwenye uzalishaji wa kazi zao (Location) ajali,hasara hata vilevile madhara hutokea hivyo kupitia shirika letu la Bima la Taifa ( NIC) litahakikisha linagharamia hasara yoyote itakayotokea."
Mdenye ametoa ushauri kwa wasanii hao kujiunga kwenye bima hiyo ili waweze kutengeneza kazi zao kwa amani na kwa uhalisia zaidi kwani wengi wanakumbwa na kadhia ya kuhofia kuharibu vitu vya gharama wawapo kwenye maeneo ya matukio ( Location).
"Bima ya kinga ya Ajali (Personal Accident insurance )kwakuwa wanasafiri sana Bima hii itawalipa fidia pale wanapoumia katika shughuli zao ".
Mdenye ameongeza kuwa bima hiyo muhimi kwani kuna Filamu ambazo ni za hatari wakati wa kutengeneza hivyo wasanii hao wanaweza kupata ajali na kuumia bima hiyo itafanya huduma ya kuhakikisha Msanii anapata matibabu ya haraka.
Meneja wa Shirika la Bima la Taifa Moshi Mkoani Kilimanjaro John Mdenye akizungumza na wasanii pamoja na wadau wa Filamu katika semina fupi juu ya usimamizi mzuri wa fedha huku akiwasihi wasanii kuhakikisha wanapata huduma za kibima hususani bima ya Ajali (Personal Accident insurance) yenye kumpa tafu Msanii akipata tatizo la Ajali au madhara ya kitu awapo kwenye eneo la kazi zake .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...