Na Khadija Seif - Michuzi TV Arusha
Zimebaki saa chache kufikia Fainali ya Tamasha la tuzo za Filamu nchini ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na michezo Mohamed Mchengerwa Kesho Disemba 17,2022 ukumbi wa Kimataifa AICC Jijini Arusha.
Akizungumza na Michuzi TV Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt.Kiagho Kilonzo wakati wakufunga semina fupi ya usimamizi wa fedha kwa wadau wa Filamu nchini ameeleza kuwa Maandalizi ya Fainali ya Tamasha la tuzo za Filamu yanaendelea vizuri huku akiwataka wasanii kuwa kitu kimoja na kutengeneza kazi nyingine nyingi zenye ubora baada ya tuzo hizo wasilewe sifa.
Aidha katika Semina hiyo imeshirikisha viongozi wa Bodi ya Filamu, Shirika la bima la Taifa (NIC) pamoja na wasanii wakiwemo waandaaji wa miswada(script), watayarishaji wa filamu pamoja na viongozi wa Mashirikisho.
"Katika Semina,mdahalo na Kongamano ndio sehemu pekee unaweza pata maoni,ushauri ya wasanii wako hivyo semina hii imetoa fursa kuwasikia wasanii wana maoni yapi kwa sababu usipowapa nafasi wanaweza kwenda kwenye mitandao ya kijamii wakaandika vitu ambavyo kiungwana tungweza kukaa nao na kukusanya kero zao na kuzipatia ufumbuzi wa haraka zaidi. ''
Aidha,Kilonzo ameeleza kuwa lengo la semina hiyo pia zaidi katika usimamizi wa fedha kwa wasanii na namna ya kutumia bajeti katika kutengeneza kazi zenye ubora na zenye viwango vinavyokidhi soko la Filamu ndani na nje.
"Bodi ya Filamu kama walezi tumekua tukipokea malalamiko mengi kutoka kwa wanunuaji wa kazi za wasanii wakiwemo Azam,Dstv pamoja na Startimes wakiwalalamikia wasanii kuwa wamelipwa fedha kwa ajili ya kutengeneza tamthilia badala yake hatoi mrejesho mzuri kwao pamoja na wasanii kupata changamoto ya kutolipwa fedha zao hususani kwa watayarishaji hivyo elimu hiyo imewafungua zaidi namna ya kufanya usimamizi mzuri wa fedha. "
Hata hivyo Kilonzo amesema tayari maandalizi yamekamilika kwa 100% kuelekea fainali ya tuzo hizo huku akiwataka wasanii kuendelea kupiga kura kwa vinyang'ayiro wanavyoshindania.
Pia amesema amepokea ombi la wasanii wa visiwani zanzibar kuomba tuzo hizo kwa mwakani kufanyika zanzibar kutokana na kuwepo kwa vivutio vingi vya utalii ndani ya visiwa vya marashi ya karafuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...