.Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imefanya mafunzoya unywaji pombe kistarabu na uendeshaji vifaa vya moto katika kuelimisha watumiaji wa vyombo  vya moto juu ya usalama barabarani  ambapo nchi inaingia katika msimu wa sikukuu unaokuwa na shamra shamra nyingi.

Mafunzo hayo yamefanyika katika viwanja vya Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kujumuisha ushiriki wa zaidi ya madereva 100 wa pikipiki,bajaji, polisi Tanzania na wafanyakazi wa SBL.

Takwimu zinaonyesha ajali za barabarani ni moja ya chanzo kikuu cha vifo Tanzania na barani Afrikaikiwa sababu kubwa kuwa uzembe barabarani, mwendo mkali na kuendesha vyombo vya moto wakati umelewa. Matukio haya huzidi katika msimu wa sikukuu hivyo elimu ya usalama barabarani ni muhimu kwa watumiaji wote.

Katika msimu huu, SBL na jeshi la polisi wameelimisha madereva kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuacha kuendesha vyombo vya moto wakiwa wametumiwa kilevi .

Madereva magari,waendesha pikipiki na bajaji wameelimishwa juu ya unywaji kwa kiasi na kuaswa kuwa mabalozi wa usalama barabarani kwa wenzao na watumiaji wengine wa barabara.

Mkurugezi wa Masoko wa SBL  Anitha Msangi Rwehumbiza amesema, “Kupitia ushirikiano huu na Jeshi la Polisi Tanzania tunategemea  madereva magari na pikipiki tuliowapa mafunzo watakuwa mabalozi wazuri hasa katika kipindi hiki cha sikukuu ambapo tumewahimiza kutokunywa na kuendesha vyombo vya moto. Madereva wetu wote wanajukumu la kuhakikisha abiria wao wamefika katika maeneo wanayokwenda salama”

SBL ilionyesha video na kucheza vipindi vya kuelimisha kuwapa madereva elimu ya usalama barabarani. Zaidi ya hilo, SBL iliendelea kuwapa nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa ili kuangalia kiwango cha uelewa wao.

Pia, SBL imetumia nafasi hiyo kutanua wigo wake kwa umma hasa katika kufurahia bidhaa zake na kunywa kwa kiasi, kunywa maji katikati ya unywaji pombe na kuwa na dereva maalum (asiyelewa) au taxi na kutoendesha wakati wamelewa.

“Umma unahamasishwa kutembelea uwanja wa Drink IQ wa SBL uliopo katika mtandao unaopatikana katika vifaa vyote. Drink IQ ni mfumo wa kieletroniki unaopatikana kwa Kiswahili na Kingereza. Mfumo huuu unatoa taarifa kuhusu viwango na aina ya vimiminika vilivyopo katika bidhaa za SBL, kiwango cha kuhimili pombe, mbinu za kufuatilia unywaji wa pombe, ukweli na mambo ya kuzusha yanayohusu matumizi ya pombe” Anitha aliongezea.

Mwanasheria wa Kikosi na Mkuu wa Dawati la Elimu Traffiki Makao Makuu, Kamanda Deus Sokoni alifurahishwa na juhudi za SBL katika kuelimisha madereva boda boda na bajaji kuhusu usalama barabarani hasa katika kipindi hiki cha sikukuu.

“Niwapongeze SBL kwa jitihada hii kwa sababu inavutia na kuhusisha kila mdau. Mafunzo haya nina amini kabisa yatazuia ajali zisizokuwa na msingi na matukio mbalimbali  ya barabarani katika kipindi hichi cha siku kuu.” Alisema Kamanda.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...