NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza imeanika mikakati ya kuzuia vitendo vya rushwa kwa mujibu wa sheria ili thamani ya fedha za umma ionekane kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, James Ruge alisema jana wakati akitoa kwa waandihi wa habari taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo kwa robo ya kwanza kuanzia Julai hadi Septemba 2022.
Amesema katika robo ya pili ya Oktoba hadi Disemba 2022, TAKUKURU mkoani Mwanza itendelea kutekeleza ajuumu yake kkwa mujibu wa sheria.
Ruge amesema katika kuzuia rushwa kwenye miradi ya maendeleo itakagua na kusimamia kwa karibu matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa na serikali kutekeleza mirdi hiyo ili thamani ya fedha hizo ionekane.
Amesema mkakati wa pili ni kuchunguza makosa kwa wot watakaojihusisha na vitendo vya rushwa na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.
“Elimu yaa mapambano dhidi ya rushwa itatolewa zaidi kupitia vyombo vya habari (redio,magazeti, luning na mitandao ya kijamii) na utaratibu wa TAKUKURU inayotembea katika kuhakikisha inawafikia wananchi moja kwa moja katika maeneo yao na kuwaelimisha umuhimu na wajibu wao kusimamia miradi ya maendeleo ,”amesema Ruge.
Amesema anaamini njia hiyo itaongeza na kupanua wigo wa ushirikishaji wananchi katika kuzuia na kupambana na rushwa kama ilivyo kauli mbiu ya mapambano dhidi ya rushwa ‘Kuzuia Rushwa ni Jukumu langu na lako; Tutimize Wajibu Wetu.’
Amefafanua kuwa kauli mbiu hiyo ni muhimu na wananchi wanapaswa kuibeba na kuwaasa kujiepusha na rushwa pamoja na kuwafichua wanaotumia nafasi zao kujinufaisha binafsi kwa rushwa ili wachukuliwe hatua.
Aidha amesema Jamhuri imeshinda kesi tisa zilizofunguliwa mahakamani na taasisi hiyo kati ya kesi 11 huku watumishi wa umma wa serikali za mitaa waliokuwa wakijihusisha na ukusanyaji wa mapato wakiguswa na mkono wa sheria kwa kutiwa hatiani,imefungua kesi mpya tisa,27 zinaendelea kusikilizwa ambapo majalada matano yalyopelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) yakipata kibali na watuhumiwa watfikishw mhakamani punde.sss
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza,James Ruge,leo akitoa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo katika robo ya kwanza,Julai hadi Septemba 2022.Picha na Baltazar Mashaka
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...