Katibu Tawala Mkoani Pwani,
Zuwena Omari akifungua semina ya uhamasishaji wa mradi wa Shule Bora
nchini kwa wahariri na wasimamizi wa vyombo vya habari mkoani
humo,semina ambayo imefanyika ukumbi wa Destiny Kwamatias,wilayani
Kibaha

Waandishi wa habari Mkoani Pwani
walioshiriki semina ya uhamasishaji wa mradi wa Shule Bora nchini kwa
wahariri na wasimamizi wa vyombo vya habari mkoani humo,semina ambayo
imefanyika ukumbi wa Destiny Kwamatias,wilayani Kibaha .(picha zote na
Mwamvua Mwinyi)

Mwenyekiti wa Chama Cha waandishi
wa habari Mkoani Pwani Ally Hengo,akieleza Jambo katika semina ya
uhamasishaji wa mradi wa Shule Bora nchini kwa wahariri na wasimamizi wa
vyombo vya habari mkoani humo,semina ambayo imefanyika ukumbi wa
Destiny Kwamatias,wilayani Kibaha


Ofisa elimu mkoa wa Pwani Sara
Mlaki akizungumza katika semina ya uhamasishaji wa mradi wa Shule Bora
nchini kwa wahariri na wasimamizi wa vyombo vya habari mkoani
humo,semina ambayo imefanyika ukumbi wa Destiny Kwamatias,wilayani
Kibaha.
…………………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Disemba 8
WAANDISHI wa habari
wameaswa kutumia nguvu ya kalamu zao kuandika taarifa za mradi wa Shule
Bora ,mpango ambao unalenga kuweka mikakati na kutafuta suluhisho kwa
watoto wa makundi maalum ,wakike na wale wa kiume wanapata elimu iliyo
kwenye mazingira bora.
Aidha waandishi hao
wametakiwa kushirikiana na Serikali na vitengo vya elimu ili kuweza
kupata taarifa mbalimbali na zilizo sahihi.
Katibu Tawala Mkoani
Pwani, Zuwena Omari akifungua semina ya uhamasishaji wa mradi wa Shule
Bora kwa wahariri na wasimamizi wa vyombo vya habari mkoani humo
,alieleza wanaendelea kuimarisha mahusiano baina ya Serikali na vyombo
vya habari ili mradi ulete tija .
“Hakuna asiyejua
nguvu ya kalamu za waandishi wa habari,kwa kuandika taarifa
zinazoaminika kwenye kampeni za maendeleo nchini,Sisi Kama mkoa
tutaimarisha mahusiano na vyombo vya habari ili kuhakikisha mradi
unaleta mafanikio “alifafanua Zuwena.
Akielezea mradi
,Zuwena alieleza umefadhiliwa na mfuko wa Ukaid unalenga kuunga mkono
uboreshaji wa elimu msingi Tanzania kwa miaka sita ,katika Halmashauri
67 na itahusisha watoto milioni 3.8 katika mikoa 9 inapotekelezwa mradi
ikiwemo mkoa wa Tanga ,Pwani, Dodoma, Singida, Kigoma,Katavi ,Simiyu
,Mara na Rukwa.
“Utekelezaji wa
mradi umelenga kuboresha ufundishaji kwa walimu, kuboresha elimu
jumuishi kwa makundi ya watoto wenye mahitaji maalum , kuboresha
ujifunzaji kwa wanafunzi pamoja na kuboresha mfumo wa usimamiaji wa
sekta ya elimu katika kuhakikisha kila kiongozi anawajibika ipasavyo kwa
nafasi yake ili kufikia adhma iliyokusudiwa”alisema .
Ofisa elimu mkoa wa
Pwani,Sara Mlaki alieleza mradi wa Shule Bora ulizinduliwa Kitaifa na
Kimataifa mwaka 2021 katika shule ya msingi Mkoani iliyopo Pwani .
Alieleza kwasasa
zipo kazi zinazoendelea kufanywa kulingana na matakwa ya mradi ikiwa ni
sanjali na uboreshaji wa ufundishaji darasa la 1,2 , kuimarisha
usimamizi wa shule na elimu katika Mamlaka za Serikali ya mitaa ambapo
wameshaanza kuona matokeo chanya kwa kupanda kwa ufaulu.
Mwenyekiti wa Chama
Cha Waandishi wa habari Mkoani Pwani, Ally Hengo alishukuru waandishi
kuachiwa mlango wazi kupata taarifa ama kupewa ufafanuzi juu ya masuala
ya elimu kupitia maafisa habari kwani changamoto kubwa wanayoipata ni
kukosa taarifa kwa wakati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...