NA Yeremias Ngerangera

Wakiongea kwenye mafunzo yanayofanyika katika madarasa ya shule ya sekondari Lugalo manispaa ya Iringa, mratibu wa mpango wa shule salama Hilda Mgomapayo alisema vitendo vya ubakaji kwa watoto vinaongezeka kwa kasi hivyo jitihada za maksudi za jamii zinahitajika kupinga vitendo hivyo.

Mgomapayo alisema njia sahihi ya kukomesha jambo hilo ni kuimarisha mawasiliano kati ya jamii na shule ili kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto vinavyojitokeza katika jamii ,kuimarisha stadi za maisha ,kuimarisha mfumo wa kushughulikia malalamiko pamoja na kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji.

Hata hivyo Mgomapayo alisisitiza uundaji wa mabaraza ya watoto ili kupata changamoto zinazowapata watoto ,kuunda klabu za watoto pamoja na kuweka masanduku ya maoni .

Naye Rugarata Mwashemi kutoka ofisi ya Raisi Tamisemi aliwaambia washiriki wa mafunzo kuwa lengo la mpango wa boost ni pamoja na kuongeza uandikishaji wa watoto wa elimu awali ili waweze kupata elimu inayostahili katika umri wao wa miaka 3 mpaka 5.

Mwashemi alisema Ili kufanikisha zoezi la uandikishaji ni lazima pia kuwatengenezea mazingira mazuri ya kupata elimu hiyo na kinyume cha hapo watoto hao watakwazika na mazingira yaliyopo shuleni na kuwafanya wasipende masomo kutokana na mazingira yasiyorafiki kwao.

Aidha aliwaagiza washiriki mafunzo hayo kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa elimu ya awali na kuhakikisha kwamba watoto wote wanaoandikishwa kujiunga na elimu awali wanakamilisha mafunzo yao.

Ally Swalehe mratibu wa mafunzo ya boost kutoka ofisi ya Raisi TAMISEMI alisema Boost ni mpango wa kulipa kulingana na matokeo na katika mpango huo serikali inatarajia kutumia shilingi trilioni 1.15 kutekeleza miradi kwa kipindi cha miaka mitano.

Swalehe alidai katika miradi ya miundombinu serikali inatarajia kujenga madarasa 12,000 na shule salama 6,000 pamoja na kuviwezesha vituo teule vya walimu na Shule shikizi vituo 800 kuwa na uwezo wa kutumia Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA)katika shule hizo .

Mafunzo ya Boost yametolewa kwa muda wa siku mbili ambapo washiriki zaidi ya 280 kutoka katika mikoa ya Ruvuma,Njombe na iringa wameaswa kwenda kuzingatia utawala bora katika utekelezaji wa majukumu yao.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...