USHIRIKIANO na umoja wa Taasisi mbalimbali ni kitu mhimu katika kuleta maendeleo ya nchi na wananchi wenyewe.

Hayo yamesemwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Godbertha Kinyondo leo Desemba 30, 2022 wakati wa kusambaza matokeo ya Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe juu ya Hifadhi za jamii kwa wafanyakazi wa sekta zisizo rami kwa wakazi wa kata ya Yombo vituka, Mtaa wa Mzambarauni, Temeke jijini Dar Es Salaam. Amesema kuwa ujio wa NSSF, NHIF, Benki pamoja na vyama vya ushirikishwaji vya wananchi na watafiti umeleta maendeleo katika utoaji taarifa za hifadhi za jamii kwa wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi.

Amesema kuwa Usambazaji wa matokeo hayo umeanza kuzaa matunda kwani baadhi ya wafanyakazi sekta isiyo rasmi wamechukua fomu za kujiunga na hifadhi ya jamii ya NSSF pia amesema kuna wajasiliamali wamepata mikopo kutoka taasisi za kifedha hasa benki ya CRDB kwani baadhi ya vikundi vimetambuliwa.

Dkt. Kinyondo ameziomba taasisi za hifadhi ya jamii na taasisi za kifedha ziweze kutumia vikundi mbalimba vya wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi ili kuwapa huduma kwa njia ya vikundi vyao kwani mtu mmoja mmoja hawezi kupata huduma hiyo kiurahisi.

Pia amesisistiza mifuko ya hifadhi ya jamii kutoa taarifa juu ya huduma wanazozitoa kwa wananchi hasa wananchi wanaofanya kazi katika sekta zisizo rasmi nchini.

Amesema kuwa taasisi hizo zishirikiane na Serikali za mtaa ili kutoa elimu ya huduma wanazotoa ili kila mwananchi awe na uelewa juu ya huduma zinazotolewa kwa njia ya vikundi ili azima ya serikali ya Bima ya afya kwa wote ifanikiwe kiurahisi.

Amesema taasisi hizo zitumie watu rasmi kwa kuungana na Vikundi vya wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi kutoa elimu. Kwani wao nirahisi kukusanyana.

"Ni mhimu taarifa zitoke kwenye mamlaka za chini kwenda kwenye Mamlaka za juu ili kila mwananchi awe na taarifa juu ya huduma zinazotelewa nchini kupitia taasisi zake." Amesema Dkt. Kinyondo

Diwani wa Kata ya Yombo Vituka, Furgenzi Rwiza amewapongeza watafiti wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa kufanya tafiti zenye tija kwa jamii.

"Nimefarijika sana kwa watafiti wa Chuo Kikuu Mzumbe kufika kwenye kata yangu, Nikiombe Chuo hiki kutumia Kata ya yombo Vituka kama mfano katika kata za wilaya ya Temeke na Dar es Salaam kwa Ujumla kwa sababu kuna vijana ambao wanajitoa na wanafanya biashara ndogo ndogo kwa kujituma zaidi." Amesema

Mtafiti Chuo Kikuu Mzumbe Aloyce Gervas amesema wameendelea kusisitiza umhimu wa Kujiunga na Mifuko ya kijamii hasa Bima ya afya na Mfuko ya hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi hasa wafanyabiashara ndogo ndogo, wajenzi, Mama Rishe, baba rishe na waendesha bodaboda wa kata ya Yombo vituka, Mtaa wa Mzambarauni.

Amesema usambazaji wa matokeo ya utafiti huo imekuwa na mafanikio kwao hasa Chuo kwa Ujumla, pia amesisitiza umhimu wa sekta zisizorasmi zizidi kuheshimika na kuzidi kupewa kipaumbele katika utungaji wa sera na sheria mbalimbali za nchi.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Godbertha Kinyondo akizungumza leo Desemba 30, 2022 wakati wa kusambaza matokeo ya Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe juu ya Hifadhi za jamii kwa wafanyakazi wa sekta zisizo rami kwa wakazi wa kata ya Yombo vituka, Mtaa wa Mzambarauni, Temeke jijini Dar Es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Godbertha Kinyondo akizungumza na mwandishi wetu leo Desemba 30, 2022 wakati wa kusambaza matokeo ya Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe juu ya Hifadhi za jamii kwa wafanyakazi wa sekta zisizo rami kwa wakazi wa kata ya Yombo vituka, Mtaa wa Mzambarauni, Temeke jijini Dar Es Salaam.
Mtafiti Chuo Kikuu Mzumbe Aloyce Gervas akizungumza na mwandishi wetu leo Desemba 30, 2022 wakati wa kusambaza matokeo ya Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe juu ya Hifadhi za jamii kwa wafanyakazi wa sekta zisizo rami kwa wakazi wa kata ya Yombo vituka, Mtaa wa Mzambarauni, Temeke jijini Dar Es Salaam.
Amani Mwinyimvu kutoka TAROTU akizungumza leo Desemba 30, 2022 wakati wa kusambaza matokeo ya Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe juu ya Hifadhi za jamii kwa wafanyakazi wa sekta zisizo rami kwa wakazi wa kata ya Yombo vituka, Mtaa wa Mzambarauni, Temeke jijini Dar Es Salaam.


Baadhi ya wananchi wa Kata ya Yombo Vituka wakiuliza maswali wakati Chuo Kikuu Mzumbe wakitawanya utafiti walioufanya.
Baadi ya wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi wa Kata ya Yombo Vituka wakisikiliza Matokeo ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...