Na.Khadija Seif,Michuzi TV
KAMATI ya Tuzo za Filamu wametaja rasmi vipengele 32 pamoja na washiriki 162 watakaowania tuzo hizo 17,2022 Jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa Filamu Leo Disemba 9,2022 Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Maendeleo ya Filamu kutoka Bodi ya Filamu Emmanuel Ndumukwa amesema Serikali iliamua kuanzisha tuzo hizi kwa lengo la kutambua mchango wa tasnia ya filamu pamoja na kutambua vipaji vilivyojificha vya wanatasnia ya filamu.
"Tuzo hizi zilianzishwa kwa lengo la kuongeza hamasa ya wanatasnia kuzalisha kazi nyingi zaidi za Filamu hivyo kuwepo kwa tuzo hizi ni kuwapa moyo sekta hii kuzalisha kazi zenye ushindani kufikia soko la Kimataifa. "
Aidha ametaja vipengele vinavyowania tuzo hizo ni Msanii bora wakike chaguo la watazamaji wasanii waliofanikiwa kuingia ni Bi stara kupitia filamu ya kombolela, Msanii bora wakike chaguo la watazamaji wasanii waliofanikiwa kuingia ni Bi stara kupitia filamu ya kombolela, Wema Sepetu filamu ya "Malkia,Hidaya Njaidi filamu ya "moyo", Thecla mjata "Nafu'', Frola Mvungi filamu ya "Mwanahawa" pamoja na Chuchu hansy filamu yake ya "Beki tatu.
Kipengele cha Msanii bora wakiume chaguo la watazamaji waliofanikiwa kuingia ni kipengele cha Msanii bora wakiume chaguo la watazamaji waliofanikiwa kuingia ni Nkwabi Ng'wanamala maarufu kama Mzee Kikala kupitia filamu ya "Kombolela" Adam Nawanda kupitia filamu ya "Merchandizer,Ayubu Bombwe filamu ya "Alifu kwa ujiti" John kokolo kupitia filamu ya "wandongwa".
Ndumukwa amefafanua zaidi kuwa wasanii waliofanikiwa kupita kwenye kinyang'anyiro hicho watatembelea vivutio vya utalii Mkoa wa Kilimanjaro na Jiji la Arusha kwa ujumla.
Pia ametoa wito kwa wachekeshaji kutengeneza stori zenye muunganiko.
''Wachekeshaji bado ni wazuri, lakini hadithi au story zao zinakosa muunganiko wa ule ucheshi kuzingatia maeneo ambayo Wachekeshaji wazuri hawaonekani au kutokea basi kipande hicho kinakosa ucheshi. "
Kwa upande zamaradi Nzowa moja ya waratibu wa tuzo za Filamu amesema kura zitapigwa kwa njia mbili kupitia mfumo wa ujumbe mfupi pamoja na kupitia mfumo wa tovuti ukiambatanisha na code ya msanii au kazi unayoipigia kura .
Nae Msanii Neema walele ametoa pongezi kwa waandaji wa tuzo hizo kwa kuratibu zoezi la mchujo bila upended wala kuangalia ukongwe kwenye tasnia ya filamu.
"Nipongeze zaidi waratibu wa tuzo hizi kazi yangu ndio ya kwanza kutengeneza lakini nilipoamua kuingiza kwenye mchakato huu nimefanikiwa japo katika mchuano huo vipengele nilivofanikiwa kuingia kuna wakali zaidi yangu ambao wamenitangulia katika tansia."
Aidha amewaomba wadau wampigie kura kwa wingi ili waweze kumpa ushindi na kuendelea kutengeneza kazi nzuri zitakazoweza kuingia katika soko la Kimataifa na mitandao mbalimbali ikiwemo Netflix.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...