Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas (kushoto) akisalimiana na na maofisa waandamizi wa benki ya Exim akiwemo Menejea wa Benki hiyo tawi la Mtwara Bw George Mmangi na Mkuu wa Kanda wa benki hiyo Bi Elezabeth Mayengo pamoja na wageni waalikwa alipowasili kwa ajili hafla fupi ya uzinduzi wa tawi jipya la benki ya Exim mkoani Mtwara baada ya kuhamishiwa katika jengo la Sokoine House (PSSSF) katikati ya Manispaa ya Mtwara. Uzinduzi huo umefanyika mapema hii leo mkoani humo na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo mkoani humo wakiwemo viongozi wa serikali na wateja wa benki hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas (wa pili kulia) akiwa tayari kukata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la benki ya Exim mkoani Mtwara baada ya kuhamishiwa katika jengo la Sokoine House (PSSSF) katikati ya Manispaa ya Mtwara wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika mapema hii leo mkoani humo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw Dunstan Kyobya (Kulia) na Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa Benki ya Exim, Bi Agnes Kaganda, wageni waalikwa pamoja na maofisa wa benki hiyo.
Tujipongeze!
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw Dunstan Kyobya (Kulia) wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa Benki ya Exim, Bi Agnes Kaganda (Kushoto) alipokuwa akielezea muoenekano wa tawi jipya la benki hiyo mkoani Mtwara baada ya kuhamishiwa katika jengo la Sokoine House (PSSSF) katikati ya Manispaa ya Mtwara wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika mapema hii leo mkoani humo. Wa pili kushoto ni Meneja wa tawi hilo Bw George Mmangi.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas (alieketi) akifuatilia maelekezo kutoka Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa Benki ya Exim, Bi Agnes Kaganda (Kulia) wakati Mkuu huyo wa Mkia akifungua akaunti yake kupitia benki hiyo wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la benki ya Exim mkoani Mtwara baada ya kuhamishiwa katika jengo la Sokoine House (PSSSF) katikati ya Manispaa ya Mtwara wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika mapema hii leo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas akizumgumza na wafanyakazi wa benki ya Exim pamoja na wateja wa benki hiyo wakati wa hafla hiyo.
Akizungumza kwenye ya hafla hiyo Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa Benki ya Exim, Bi Agnes Kaganda (pichani) alisema uamuzi wa kuboresha zaidi tawi hilo unalenga kuunga mkono jitihaza za serikali za kukuza uchumi wa mkoa huo kupitia uwekezaji mkubwa kwenye upanuzi wa huduma za bandari na kuboresha hali ya kilimo hatua ambayo inachochea ukuaji wa biashara ya ndani na ile ya kimataifa hususani kati ya Tanzania na Comoro.
Akizungumza kwenye ya hafla hiyo Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa Benki ya Exim, Bi Agnes Kaganda (pichani) alisema uamuzi wa kuboresha zaidi tawi hilo unalenga kuunga mkono jitihaza za serikali za kukuza uchumi wa mkoa huo kupitia uwekezaji mkubwa kwenye upanuzi wa huduma za bandari na kuboresha hali ya kilimo hatua ambayo inachochea ukuaji wa biashara ya ndani na ile ya kimataifa hususani kati ya Tanzania na Comoro.
Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Mtwara Bw Georgee Mmangi akizunguna na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.Hafla ya uzinduzi huo ilihudhuliwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo mkoani humo wakiwemo viongozi wa serikali na wateja wa benki hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya Exim, wageni waalikwa na wateja wa benki hiyo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa tawi jipya la benki ya Exim mkoani Mtwara baada ya kuhamishiwa katika jengo la Sokoine House (PSSSF) katikati ya Manispaa ya Mtwara. Uzinduzi huo umefanyika mapema hii leo mkoani humo.
Muonekano wa tawi jipya la benki ya Exim mkoani Mtwara baada ya kuhamishiwa katika jengo la Sokoine House (PSSSF) katikati ya Manispaa ya Mtwara.
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amewaomba wafanyabiashara mkoani
humo kuchangamkia fursa za kibiashara baina ya mkoa huo na nchi jirani
ikiwemo Comoro huku akiipongeza Benki ya Exim Tanzania kwa kuwa mstari
mbele katika kufanikisha huduma za kifedha baina ya Tanzania na visiwa
hivyo.
Akizungumza mapema hii leo wakati hafla fupi ya uzinduzi
wa tawi jipya la benki ya Exim mkoani Mtwara lililohamishiwa katika
jengo la Sokoine House (PSSF) katikati ya Manispaa ya Mtwara, Kanali
Abbas alisema licha ya uwepo wa fursa za biashara kutokana na mahitaji
ya bidhaa za chakula ikiwemo maharage, nyama, ulezi na ufuta nchini
Comoro changamoto ilibaki kuwa ni huduma za kifedha baina ya mataifa
hayo mawili.
Alisema jitihada za benki ya Exim kuboresha huduma hizo utatatua changamoto hiyo.
“Nimefurahi
kusikia kwamba benki ya Exim ina matawi zaidi ya matano nchini Comoro
na ndio benki inayoongoza kwa ukubwa nchini Comoro na leo hii tunazindua
tawi lao jipya na la kisasa zaidi hapa Mtwara. Jitihada hizi za Exim
ndio zinanipa nguvu ya kuwashawishi zaidi wafanyabiashara mkaoni Mtwara
na maeneo jirani kutumia vema fursa hii kwa kuwa uhakika wa huduma za
kifedha sasa upo…tunawashukuru sana benki ya Exim.’’ Alisema.
Kwa
mujibu wa Kanali Abbas uzinduzi wa tawi hilo umekuja wakati muafaka
kipindi ambacho mkoa huo unatarajia ugeni wa viongozi wakubwa kutoka
nchini Comoro watakaoambatana na idadi kubwa ya wafanyabiashara kutoka
nchini humo ili kuja kujionea fursa za biashara baina ya mataifa haya
mawili.
Awali akizungumza kwenye ya hafla hiyo Mkuu wa Idara ya
Mtandao wa Wateja wa Benki ya Exim, Bi Agnes Kaganda alisema uamuzi wa
kuboresha zaidi tawi hilo unalenga kuunga mkono jitihaza za serikali za
kukuza uchumi wa mkoa huo kupitia uwekezaji mkubwa kwenye upanuzi wa
huduma za bandari na kuboresha hali ya kilimo hatua ambayo inachochea
ukuaji wa biashara ya ndani na ile ya kimataifa hususani kati ya
Tanzania na Comoro.
“Baada ya kuona jitihada hizo za serikali na
kwa kuheshimu wateja wetu tukaona ni vema tuwafungulie tawi lenye hadhi
wanayostahili. Tawi hili pia linaendana na mabadiliko makubwa ya huduma
za kisasa za kibenki zinazohusisha matumizi ya teknolojia ya hali ya
juu katika utoaji wa huduma za kifedha.’’ alisema.
Kwa mujibu wa
Bi Kaganda benki hiyo tayari imejipanga kuwahudumia wateja wake
wakiwemo wafanyabiashara baina ya Tanzania na Comoro ambapo hivi
karibuni ilizindua rasmi huduma yake mpya ya kibenki isiyo na mipaka
kati ya mataifa hayo mawili ikilenga kutoa miamala ya gharama nafuu kwa
wateja na wafanyabiashara hao.
“Kupitia huduma hii isiyo na
mipaka, raia wa Comoro anayetembelea Tanzania kwa sababu za biashara,
matibabu au madhumuni yoyote anaweza kutoa fedha au kufanya malipo ya
huduma hizo wakati wowote akiwa hapa nchini bila kuathiriwa na sababu za
kimipaka baina ya mataifa haya mawili.’’
"Wanachohitaji wateja
ni kutembelea matawi yetu mahususi kwa ajili ya huduma hii yaliyopo Dar
es Salaam, Zanzibar na hili la hapa Mtwara na hivyo kuwarahisishia
kufanya biashara na kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari na usumbufu wa
kufanya biashara kwa fedha taslimu,'' alibainisha.
Akizungumza
kwa niaba ya wateja wengine wa benki hiyo mkoani Mtwara, Bw Henry Shimo
pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa huduma nzuri na heshima
inayoendelea kuitoa kwa wateja wake mkoani humo, aliiomba iendelee
kuboresha upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu zaidi kwa wakazi wa
mkoa huo wanaotegemea kilimo, uvuvi na biashara ili waweze kunufaika
zaidi na jiografia ya mkoa huo unaopakana na mataifa ya Msumbiji na
Comoro.
Hafla ya uzinduzi huo ilihudhuliwa na wadau mbalimbali
wa benki hiyo mkoani humo wakiwemo viongozi wa serikali na wateja wa
benki hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...