Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Iddi Kajuna ametoa baraka zake kuelekea uchaguzi wa Klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika Januari 29, 2023, Kajuna amewatoa hofu Mashabiki wa Klabu hiyo na kuwaomba kuungana kwa pamoja kuchagua Viongozi bora zaidi wenye weledi na wenye kujua vizuri michezo hususani mpira wa miguu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Kajuna amemtaja Mama Asha Baraka ambae anagombea nafasi ya ujumbe kwa upande wa Wanawake, amemtaja Asha Baraka ni mgombea mwenye mapenzi ya kweli na Klabu na amekuwa katika Sekta ya Michezo kwa muda mrefu.

Kajuna amesema ana imani na Asha Baraka endapo atachaguliwa katika nafasi hiyo ya Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi kama Mwanamke ambaye alikuwa mstari wa mbele katika harakati za kuipigania timu ya Simba na timu ya Wanawake ya Simba Queens.

“Asha Baraka tulikaa naye kuweka mipango mizuri wakati wa maandalizi ya mechi yetu dhidi ya Yanga, Kigoma na tuliweka heshima ya kumfunga Yanga kwenye Fainali ya Kombe la Shirikisho, kwa hiyo tunamjua vizuri, na kwenye kundi la Wanaume wanne, Mwanamke mmoja hawezi kuathiri kitu chochote wala hakuna kitakachoharibika,” amesema Kajuna.

Katika Uchaguzi huo wa Simba SC, kuna jumla ya Wagombea 14 wakati wagombea nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu wapo wawili na Wajumbe 12 watachuana katika kuwania nafasi ya ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu hiyo huku wakitakiwa Wajumbe watano pekee kati hao 12, huku Mwanamke mmoja lazima awepo kati ya hao Wajumbe watano.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...