Ikiwa zimesalia siku 3 tu kuelekea ‘Grand finale ‘ ambapo tutashuhudia wateja 8 wakijishindia safari ya kwenda Dubai kwa siku 4 huku benki ya NMB ikiwalipia kila kitu, benki hiyo iliendesha droo ya wiki ya mwisho ya kampeni ya NMB #MastaBataKoteKote katika Manispaa ya Morogoro kwenye tawi la NMB - Wami
Kwenye droo za kila wiki, washindi 75 wamekuwa wakinyakua TZS 100,000 kila mmoja na wa 76 akishinda pikipiki aina ya Boxer. Hii imepelekea jumla yao katika droo zote 10 za kila wiki kuwa 760.
Thamani ya zawadi walizoshinda ni pamoja na TZS milioni 75 pesa taslimu kwa washindi 750 na TZS milioni 30 za Boxer 10. Jumla ni TZS milioni 105 na thamani ya zawadi zote za shindano hili la kuchagiza malipo kidijitali ni zaidi ya TZS milioni 300.
Kabla ya zoezi la kuwapata washindi wa mwisho 76 wa kila wiki, Meneja wa Tawi la NMB Wami, Bw Harold Lambileki, alisema droo ya kuwapata washindi wa kwenda Dubai itafanyika makao makuu ya benki hiyo wiki ijayo jijini Dar es Salaam.
Meneja huyo alisema kila mteja wa NMB anayefanya miamala yake kwa kutumia NMB Mastercard na Lipa Mkononi (QR) anayo nafasi ya kushinda zawadi ya safari ya Dubai huku wanaochanja sana na kulipa zaidi kidijitali wakiwa na nafasi kubwa ya kuibuka kidedea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...