Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Imani Kajula amekuja kuiongoza Klabu hiyo kwa kasi kubwa baada ya kuanika mipango kabambe ya maendeleo ili kufanikisha malengo ya timu hiyo kufika mbali zaidi kimaendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu

Akizungumza mbele ya hadhara ya Wanachama wa timu hiyo katika Mkutano Mkuu uliofanyika jijini Dar es Salaam, Kajula amesema hataweza kufanya kazi hiyo ya kusongesha gurudumu la maendeleo peke yake bali anahitaji msaada wa wanachama, mashabiki na hata viongozi wapya watakaochaguliwa kwenye Mkutano huo.

“Nashukuru sana Bodi kuniteua, na Mwekezaji MO dewji ambaye nilipata fursa kuzungumza naye, na Mwenyekiti wa Bodi, kimsingi tupo pamoja, sasa hatua ni watu na watu ni sisi, la kwanza sisi ni Simba SC tunaoamini kwenye Nguvu Moja tuhakikishe ushirikiano ili kupata maendeleo,” amesema Kajula 

“Ninyi wanachama ni roho ya Simba SC, sio moyo, bila ninyi hakuna Simba cha kwanza kuboresha mawasiliano, tutahakikisha tunawasikiliza, tutaimarisha Matawi, tutajenga mfumo endelevu”, ameeleza Kajula.

Kajula amesema timu imara ni ile ambayo inashinda Makombe, tunaamini tutafanikisha hilo na tutajenga Taasisi imara na endelevu, tuna malengo pia ya kujenga Chapa imara ili tuweze kuongeza mapato zaidi

“Malengo mengine ni kujenga Hosteli za kisasa za Klabu, na miundombinu bora, na leo niseme tu sisi Simba SC tunasema na kutenda, lengo kupiga hatua uwanda wa Afrika na hata nje ya Afrika,” amesema Kajula.

“Ligi ya Mabingwa Afrika, mwaka huu tupo kwenye hatua ya makundi, lengo letu kufika Robo na zaidi ya hapo, hapa tuwapongeze na tunaahidi kuboresha zaidi timu ya Wanawake (Simba Queens) tumekuwa wanne Afrika naamini mbele kuna dira na nuru kubwa kwa timu yetu ya Wasichana,” ameeleza Kajula.

Hata hivyo, Kajula amesema usajili wa Wachezaji utakuwa mkubwa na wa hali ya juu, amesema wanaamini ili kuwa Mabingwa Afrika lazima wasajili vizuri na kuwa na Wachezaji wenye viwango vya hali ya juu, hivyo gharama ya usajili lazima ipande kwa kutenga fungu la usajili huo.

“Timu yetu ya wanaume, malengo ni kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, timu ya Wanawake kufika hadi Fainali ya Kombe la Afrika kwa Wanawake na kuboresha timu za vijana U-17 na U-20 zote ziwe kwenye mstari mzuri na kufanya vizuri zaidi, tunaamini kuandaa vijana tunaweza kuwa timu bora ya wakubwa”, amesema Kajula.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...