Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV-Kilosa
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Katibu Mkuu wake Daniel Chongolo kimeishauri Wizara ya Kilimo kuweka mfumo mzuri ambao utawezesha Skimu ambazo zinajengwa katika maeneo mbalimbali kuwa na tija ikiwemo kuwepo kwa Mameneja ambao watakuwa wasimamizi wa Skimu hizo ambazo ujenzi wake unatumia fedha nyingi za Serikali.
Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro leo Januari 30 mwaka 2023 ,Chongolo ametumia nafasi hiyo kueleza fedha nyingine nyinyi zimepelekwa kujenga Skimu za umwagiliaji nchi nzima na Kilosa wamenufaika na skimu mbili huku akifafanua mkoa wa Morogoro ni wanufaika wakubwa wa fedha zinazokwenda kujenga skimu.
“Hatutaweza kufanikiwa sana kwenye hizi Skimu za umwagiliaji zinazojengwa sasa kama tutaacha ziendeshwe kwa mfumo uliondeshwa wakati uliopita ili skimu hizi ziwe na tija lazima kuwe na Mameneja ambao watakuwa wanazisimamia ili kuondosha utaratibu wa kukodisha yale mashamba au yale maeneo kwa wananchi na badala yake ndani ya skimu ile kutoa utararibu mzuri.
“Kwa hiyo kazi ya msingi ni Wizara ya Kilimo kujielekeza kwenye kuweka Mameneja na mameneja hao wawe ni watalaamu wa ufundi na usimamizi wa hizo skimu na sio vinginevyo. Lakini fedha nyingi zimekuja kwa mfano kilosa mna skimu hapa mbili, sasa hivi skimu ikisumbua au ikitokea changamoto mtalaam wa kurekebisha anatoka mbali , lazima Wizara iweke utaratibu wa kuwa na Mainjinia wa umwagiliaji kwenye Wilaya zote zinahusika na kilimo cha umwagiliaji.
“Na mikoa mikubwa hasa ile ambayo ina uzalishaji mkubwa wa chakula ukiwemo Mkoa wa Morogoro ambao uko kwenye orodha ya mikoa mitano inayolisha nci yetu lazima kuwepo na Mhandisi ngazi ya Mkoa ambao kazi yao itakuwa kuratibu na kusimamia miundombinu ya umwagiliaji ndani ya mkoa husika. Tukifanya hivyo tutakuwa tunasaidia dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha fedha inayokwenda kwenye hizi skimu inawasaidia wananchi,”amesema Chongolo.
Kuhusu changamoto ya mashamba ambayo yametolewa na Serikali kwa ajili ya wananchi, Chongolo amewaahidi wananchi wa Kilosa kwamba Waziri wa kilimo Hussein Bashe atakwenda kwa ajili ya kukutana na wananchi na kisha kuwasikiliza ili kuangalia njia nzuri ya kumaliza changamoto iliyopo.
“Malalamiko yenu ni mashamba mmesema yako yaliyorudishwa kwa wananchi suala ni namna yanavyotumika , mimi nitaagiza Waziri aje huku kuzungumza na ninyi ili utaratibu namna ya kufanya kilimo na hiyo ndio kazi ya watendaji na viongozi kwenye sekta mbalimbali kila mmoja kwenye sekta yake lazima awajibike moja kwa moja kwa wananchi.
“Niwahakikishie ndani ya wiki moja Waziri atapita hapa , na maeneo mengine yenye changamoto ya miundombinu au maeno ya kilimo, hiyo ndio kazi ya Serikali kwani kazi yake sio kuacha wananchi wanalalamika na yenyewe inaenda peke yake lazima twende sambamba.Nimeaambiwa kuna wengine wamelipia na mashamba .
“Sasa niwaambie akija Waziri moja ya jambo ambalo nitamwambia angalie ni pamoja na nani kalipa na utaratibu ukoje, kisha toe maelekezo.Najua jambo hili linahitaji muda na Waziri akija atasikiliza na hata tubakibaini wanahitajika kuja zaidi ya mawaziri wawili au watatu tutamuomba Rais Samia Suluhu Hassan awaruhusu waje kushughulikia changamoto , imeonekaa mmekaa mkao wa kutaka kulima sasa kwanini mkwamishwe na mambo madogo madogo.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...