MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) amesema  uorodheshwaji wa hatifungani ya Benki ya KCB yaani KCB Fursa Sukuk, ni miongoni mwa sehemu ya maendeleo katika sekta ya fedha hapa nchini na inaweka historia ya kuwa hatifungani ya kwanza inayokidhi misingi ya Shariah kutolewa kwa umma na kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, na ambayo imeidhinishwa na Mamlaka hiyo.


Akizungumza Januari 13,2023 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa hatifungani inayokidhi misingi ya shariah kwenye soko la hisa la Dar es Salaam ,Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo Nicodemus Mkama amesema Oktoba 25, 2022 CMSA ilidhinisha Benki ya KCB kuuza hatifungani inayokidhi misingi ya shariah.

"Yaani KCB Fursa Sukuk, yenye thamani ya Sh. bilioni 10 na ongezeko la Sh.bilioni 5.Idhini ilitolewa na CMSA baada ya Benki ya KCB kukidhi matakwa ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Sura ya 79 ya Sheria za Tanzania. Pia na Miongozo ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya Utoaji wa Hatifungani ya mwaka 2019 ambapo pamoja na mambo mengine, KCB ilitakiwa kuwa, Waraka wa Matarajio wa utoaji wa hatifungani ya Fursa Sukuk.

"Kuidhinishwa na Bodi ya Ushauri wa Shariah (Shariah Advisory Board) ya benki ya KCB na kupata ithibati kutoka kwa kampuni yenye utaalam kuhusu uwekezaji unaokidhi Misingi ya Shariah.Benki ya KCB ilikidhi matakwa haya kwa kuwa na Bodi ya Ushauri wa Shariah ambayo ni KCB Sahl Shariah Advsory Board na ithibati ilitolewa na Kituo cha ushauri kuhusu uwekezaji unaokidhi Misingi ya Shariah."

Amesema Mauzo ya hatifungani ya Fursa Sukuk yalifunguliwa Novemba 9, 2022 na kufungwa  Desemba 5 , 2022, ambapo kiasi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),CPA Nicodemus Mkama 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...