Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Bw. Fadhil Maganya ameipongeza Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuandaa Mafunzo kwa Viongozi wa kamati ya Utekelezaji katika kuimarisha utendaji kazi.
Ametoa
pongezi hizo Januari 13,2023 Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati
alipotembelea eneo ambalo Mafunzo hayo yanaendelea kutolewa kwa viongozi
wa Kamati ya Utekelezaji.
Aidha
Bw.Maganya amewataka viongozi hao kuwa na upendo na kushirikiana katika
kuijenga na kuiimarisha Jumuiya na kuondoa tofauti zao pindi
zinapotokea
"Tukianza
kukwaruzana kwaruzana,hatutakwenda,tushikamane, letu liwe moja na
tuoneshe tofauti na Jumuiya zingine , utofauti uwe chanya usiwe utofauti
wa kugongana gongana ,Kamati za utekelezaji mshikamane na uongozi wenu
ufane". Amesema
Amesema
Dar es Salaam lazima iendelee kubaki ya kuigwa kwa hivyo anashukuru kwa
fursa hiyo wao hawajatengeneza baraza na wala hawana Kamati ya
utekelezaji na kamati zingine ndogo ndogo kwasababu alitaka wapate muda
kufahamiana vizuri pia .
Katika
hatua nyingine Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Taifa Bw. Fadhil
Maganya ameipa heshima Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam kujipanga
kwa pamoja katika maandalizi makubwa ya kuzindua kongamano la malezi la
Jumuiya ya hiyo mapema mwaka huu, litakaloenda nchini nzima,na kwamba
ameiomba mikoa mingine kuiga mfano wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanza
mafunzo ya uongozi kwa uharaka.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salam,
Bi.Khadija Ally amesema dhumuni la mafunzo hayo ni kuhakikisha
wanatengeneza viongozi sahihi katika nyakati sahihi ili waweze kuongoza
Jumuiya na Chama cha Mapinduzi nchini.
Pamoja
na hayo Bi.Khadija amesema kuwa katika kuelekea kwenye Uchaguzi 2024
pamoja na 2025 dhumuni la Jumuiya na Chama kwa ujumla ni kuhakikisha
wanapata ushindi kwa kishindo.
"Ushindi
wa kishindo ambao tunaenda kuupata lazima tuwe na viongozi makini ambao
wanakisi sifa na weledi katika Chama cha mapinduzi kwahiyo wametekeleza
azimio la Mkutano Mkuu wa Kumi kwa kutoa Mafunzo kwa vitendo na
tumeanza na Mkoa wa Dar es Salaam". Amesema
Hata
hivyo amemuhakikishia Mwenyekiti kwamba Mkoa wa Dar es Salaam uko
tayari kushirikiana nae bega kwa bega na kuhakikisha dira yake ya
Jumuiya ya Wazazi inang'ara na kuisimamia vyema Ilani ya Chama cha
Mapinduzi ndani ya Mkoa huo na taifa kwa Ujumla.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Bw. Fadhil Maganya akimshukuru Mwenyekiti wa Jamuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Khadija Ally kwa kuandaa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam katika kujiimarisha zaidi kwenye suala la UongoziMwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Bw. Fadhil Maganya akiteta jambo Mwenyekiti wa Jamuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Khadija Ally wakati wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Khadija Ally akizungumza wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Bw. Fadhil Maganya alipotembelea kambi ya mafunzo hayo ya siku tatu kwa Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yanayoendelea katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.Washiriki wa Mafunzo wakiendelea kusikiliza yaliyokuwa yakijiri
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Bw. Fadhil Maganya akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Washiriki wa mafunzo pamoja na Wakufunzi wa Mafunzo hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...