Picha ya Pamoja.

Matukio mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Mgahawa wa BAO.

Viongozi mbalimbali wakitembelea kuangalia namna Mgawahawa wa BAO unavyofanya kazi. 

KAMPUNI ya kampuni ya Dough Works Limited ikishirikiana na  Vivo Energy Tanzania wametengeneza zaidi ya nafasi za ajira 35 kwa wakazi ulipo mgahawa wa BAO ikiwa ni mafanikio makubwa yanayochagizwa kwa uwekezaji wa makampuni haya mawili ambayo moja kwa moja yamewanufaisha Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 11, wakati wa kuzindua Mgahawa wa tano wa BAO katika kituo cha kutolea huduma ya nishati (Mafuta) cha Engen Masaki jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dough Works Limited, Vikram Desai amesema ushirikiano huo umeleta chapa ya nyumbani ya migahawa ya BAO ambayo imeleta mafanikio mbalimbali ikiwemo mchanganyiko wa kimiminika ya kahawa ya Kitanzania na Kimataifa na zenye chaguzi zinazofaa kwa matumizi na kutoa ubora na huduma ya kiwango cha kimataifa.

Amesema Mwenendo wa ukuaji wa Migahawa ya BAO unatarajia kuendelea kukua mwaka huu wa 2023 na mipango ya maduka mengine 12 yanatarajiwa kufunguliwa katika maeneo mbalimbali yaliyochaguliwa kote nchini.

Vikram Desai, amesema kuwa matarajio ya Chapa ya migahawa ya BAO ambayo ni chapa ya Kitanzania inayojivunia na yenye uwezo wa kukua kwa kasi ikilenga kutoa huduma zenye uzoefu wa kipekee wa chakula, vinywaji na urahisi katika viwango vya juu vinavyozingatia usafi na huduma zenye ubora.

Ameeleza pia mgahawa wa BAO, unatumai kutengeneza fursa zaidi za ajira na ukuaji kwa makundi yote ya wananchi watanzania huku wakihakikisha wanafanya kazi na kununua bidhaa kutoka kwa wachuuzi na wasambazaji wa ndani ya Tanzania sambamba na kuendeleza uzoefu wa kipekee wa huduma kwa wateja.

Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Vivo Energy, Bw. Stan Mittelman, ameongeza kuwa Vivo Energy ina nia ya kuleta matokeo chanya ya kudumu kwa jamii ya watanzania.

"Kwetu sisi, hii ni zaidi ya kufanya biashara. Jukumu letu ni kufanya mambo kwa njia ifaayo, kwa kutambua uwezo kamili wa wafanyakazi wetu na tuanaoshirikiana naokibiashara, na kuhakikisha ubora unazingatiwa, usalama na uwajibikaji unakuwepo katika mazingira yote Vivo Energy ilipowekeza pamoja na kuhakikisha shughuli zetu zinakuwa endelevu.” Ameeleza

Makamu wa Rais wa Vivo Energy anayesimamia ukanda wa Magharibi na ukanda wa Bahari ya Hindi, George Roberts amesema ajenda ya ukuaji wenye kasi upo kwenye mipango yao kila siku watazidi kutengeneza fursa kwa vijana mahiri wa bara la Afrika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vivo Energy Tanzania, Bi. Khady Sene, ameshukuru jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuweka mazingira rafiki na wezeshi kwa wawekezaji na hivyo kuruhusu biashara kukua na kukuza mfumo wa utoaji ajira nchini.

Mgahawa wa BAO uliopo Engen Masaki utakuwa wazi kuanzia Jumatatu hadi Jumapili. Huduma ya kahawa utakuwa wazi kuanzia Kifungua kinywa, chakula cha mchana chenye kiwango cha juu na ubora na aina mbalimbali za vitafunio, sandwichi na milo mbalimbali itakayopatikana siku nzima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...