Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dkt. John Kalage akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Januari 26, 2023 kuhusiana na tukio la Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Kakanja iliyopo Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Isaya Benjamini ambaye alionekana kwenye kipande kifupi cha video akiwacharaza bakora kwenye nyayo za miguu wanafunzi wawili.
Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
HAKIELIMU wameipongeza Serikali kupitia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na uongozi wa Mkoa wa Kagera kwa kuchukua hatua za haraka na za awali dhidi ya mwalimu aliyehusika na ukatili lilitekelezwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Kakanja iliyopo Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Isaya Benjamini ambaye alionekana kwenye kipande kifupi cha video akiwacharaza bakora kwenye nyayo za miguu wanafunzi wawili.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dkt. John Kalage wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Januari 26, 2023. Ameipongeza pia kwa kumvua nafasi ya Ualimu Mwalimu Mkuu, kumsimamisha kazi na kuunda tume kuchunguza tukio hilo ili hatua kali za kisheria ziweze kufuatwa.
Licha ya pongezi hizo HakiElimu imepokea kwa masikilitiko taarifa za tukio la adhabu ya kikatili waliyoipata wanafunzi hao kwani kitendo hicho kinakiuka sio tu haki za Watoto bali pia ni kinyume na maadili ya kazi ya ualimu na malezi bora ya wanafunzi.
Dkt. Kalage amewaasa Walimu kutumia mbinu mbadala katika kusimamia nidhamu ya wanafunzi. Pia ameshauri kutumia vichocheo hasi ili kuwafanya wanafunzi wasiendelee na mwenendo ambao haufai badala ya adhabu ikiwemo adhabu ya viboko. Hata hivyo, matumizi ya njia mbadala kusimamia nidhamu yanategemea sana uwezo wa walimu katika kuzitumia.
Amesema Walimu wanashidwa kutumia njia mbadala na kwa sababu sheria na miongozo inaruhusu viboko basi wanachagua viboko badalla ya vichocheo hasi.
HakiElimu wametoa wito kwa serikali kuchukua hatua ambazo zitakomesha kabisa matumizi ya adhabu za viboko shuleni na kuhimiza adhabu chanya au adhabu mbadala ambazo sio za kikatili.
Pia ametoa rai kupitiwa upya kwa vipengele vya Sheria ya Elimu ya Mwaka 1978, Mwongozo wa Elimu Juu ya Adhabu za Viboko wa Mwaka 2002 na Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 ili kukataza kabisa matumizi ya viboko shuleni na kuzuia adhabu nyingine ambazo zinaweza kutoa mwanya wa ukatili unaofanyika kwa watoto.
Sambamba hayo HakiElimu imetoa mapendekeza ya kuanzishwa kwa Programu ambazo zinalenga kuondoa ukatili wa namna yoyote kwa watoto na kufanya shule kuwa mahali salama na rafiki pa kujifunzia.
Hata hivyo Dkt. Kalage ameiomba serikali Serikali kuweke mipango endelevu ya kuimarisha mifumo rasmi ya ulinzi na usalama wa watoto shuleni ikiwa ni pamoja na kuharakisha uanzishwaji wa Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto shuleni pamoja na Mabaraza ya Watoto.
Pia Serikali ichukue hatua kali dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ili kukomesha vitendo hivyo ndani na nje ya shule.
Mafunzo kazini ya walimu yanayoendelea kwa sasa yahusishe moduli inayohusu utoaji wa adhabu chanya na jinsi ya kuwarekebisha wanafunzi wenye matatizo ya kitabia kwa kushirikiana na wazazi na walimu ambapo jambo hilo napaswa kupewa kipaumbele ikiwemo kuweka bayana kikanuni wajibu wa walimu kwa wazazi.
Ukumbukwe kuwa kunavideo Fupi ilionekana zaidi wiki hii katika Mitandao ya Kijamii ambayo ilionesha Mwalimu akiwaadhibu wanafunzi kwenye Nyayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...