Mara baada ya kikosi cha Timu ya KMC FC kurejea Jijini Dar ea salaam jana, uongozi umetoa mapumziko ya siku nne kwa wachezaji na kwamba watarejea kambini Jumamosi ya Januari saba kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo mwingine dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Januari 13 katika uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.
Timu
hiyo ya Manispaa ya Kinondoni imerejea jana ikitokea Mbarali mkoani
Mbeya ambapo ilikuwa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania bara
dhidi ya Ihefu uliopigwa Januari tatu na kupoteza kwa goli moja kwa
sifuri.
Wachezaji wa KMC
FC wamepewa mapumziko hayo wakati huu Ligi ikiwa imesimama kupisha
michuano ya kombe la Mapinduzi na kwamba Jumamosi ya Januari saba Timu
itaanza mazoezi ramsi kwa ajili ya mchezo huo ambao itakuwa ugenini
dhidi ya Mtibwa Sugar.
"
Tunakwenda kwenye mapumziko mafupi wakati huu ligi ikiwa imesimama,
tumetoka kupoteza mchezo muhimu ugenini lakini bado tupo kwenye kiwango
kizuri na kwamba baada ya Timu kurejea, Kocha Mkuu Thierry Hitimana na
wasaidizi wake watafanyia kazi mapungufu waliyoyaona na hivyo kuendelea
kufanya vizuri kwenye michezo inayokuja.
Kwaupande
wa hali za wachezaji, bado kunachangamoto ya wachezaji watano ambao
wanamajeraha ambapo kati ya hao wachezaji watatu ni majeruhi wapya
waliotokana na mchezo uliopita dhidi ya Ihefu huku wawili niwale wamuda
mrefu.
Majeruhi wapya ni
Baraka Majogoro, George Makang'a pamoja na Ibrahimu Ame huku wale wamuda
mrefu ni Hance Masound Msonga pamoja na Emmanue Mvuyekure ambapo wote
wanaendelea na matibabu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...