BENKI ya Exim Tanzania imeendelea kugawa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na simu janja (smartphones) kwa washindi wa kampeni yake “Chanja Kijanja, Kimasta Zaidi’’ inayolenga kuhamasisha wateja wa benki ya Exim kutumia kadi zao za Mastercard katika manunuzi ya mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS) katika maduka mbalimbali na maeneo mengine nchini.
Kampeni hiyo iliyozinduliwa mapema mwezi Novemba inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo wanaotumia kadi zao za Exim Mastercard kufanya miamala, kuwa kwenye nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu, Simu janja (Smart Phones) na safari zilizolipiwa gharama zote kwenda mapumziko katika mataifa ya Dubai, Uturuki na Afrika Kusini wao pamoja na wenza wao.
Mkuu
wa Idara ya Huduma Mbadala Kupitia Mifumo ya Kidigitali, Benki ya Exim
Bw. Silas Matoi (wa pili kulia) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya
Iphone 14 Pro kwa Bw. Balubhai Patel (wa pili kushoto) mkazi wa jiji
la Dar es Salaam baada ya kuibuka mshindi wa droo ya pili mwezi ya
kampeni ya “Chanja Kijanja, Kimasta Zaidi’’ inayolenga kuhamasisha
wateja wa benki hiyo kutumia kadi zao za Mastercard katika manunuzi ya
mtandaoni au kufanya malipo kupitia mashine za malipo (POS).
Wanaoshuhudia ni Meneja wa benki hiyo tawi la Exim Tower Bw. Vishal
Ratansinh (kulia) na Afisa Idara ya Huduma Mbadala Kupitia Mifumo ya
Kidigitali wa benki hiyo Bw. Gregory Malembeka (Kushoto). Hafla ya
makabidhiano kwa washindi hao imefanyika jijini Dar es Salaam leo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...