Na Pamela Mollel,Arusha
Mashirika mbalimbali yasio ya kiseriklai wameiomba serikali kutenga maeneo maalum ya mifugo kwa ajili ya wafugaji ikiwa ni kuondoa migogoro ya mara kwa mara ambayo imekuwa ikijitokeza baina ya hifadhi,wakulima na wafugaji
Watendaji hao kutoka asasi 11 za kiraia wamezungumza na wanahabari jijini Arusha wakiiomba serikali kuangalia namna ya kutenga maeneo ya wafugaji ikiwa ni kuepukana na migogoro ya mara kwa mara ambayo imekuwa ikijitokeza kutokana na kutokuwa na ushirikishwaji wa wafugaji katika maeneo hayo
Loserian Maoi_Mwakilishi Shirika la Intergrated initiatives alisema kuwa migogoro hii imesababisha madhara makubwa kwa jamii zinazoishi katika maeneo hayo ikiwemo kujeruhiwa kwa wananchi
Wawakilishi hawa wa mashirika yasio ya kiserikali wanamuomba Mh Rais kukutana na kundi la wafugaji kama ambavyo amekuwa akikutana na makundi mengine ili kusikiliza changamoto zinazowakabili
Mery Mushi,Mwakilishi Shirika la Woman na Children Saport ameomba Serikali iimarishe ujirani mwema na kutoa elimu kwa wananchi wanaozunguka Hifadhi za Taifa na maeneo yote yaliyohifadhiwa
Miongoni mwa maeneo yanayotajwa kuwa na migogoro kati ya wafugaji,hifadhi na wakulima ni pamoja na loliondo,Kilosa,Wilaya ya Simanjiro ,Siha na kwingineko huku chanzo kikitajwa kuwa ni mahusiano duni kati ya baadhi ya hifadhi na wananchi wanaozunguka hifadhi hizo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...