Na Ashura Godwin , Michuzi TV Iringa 

Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa  kimetoa tamko  rasmi kuhusu  kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kufuatia tamko la Rais na  mwenyekiti wa CCM  kuruhuhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa hapa nchini, hatua inayoonesha kuwa Rais Dk.Samia ni mwana Demokrasia wa vitendo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Iringa  Daud  Yassin  amesema anaunga mkono tamko la Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na hivyo kuvitaka vyama vya siasa  kufanya  mikutano yenye amani ambayo ndio itakuwa dhamira ya Rais Dk.Samia imetimia.

"Sisi kama chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa tunatoa tamko la  kunampongeza na kumuunga mkono  Rais  kwa tamko alilitoa juu ya kuruhusu mikutano ya  Vyama vya Siasa na hivyo kunatakiwa mikutano hiyo  ifanyike kiistarabu na kuwa na tija kwa jamii"kufanya siasa za kiustaharabu na zenye tija kwa jamii" amesema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa

Amesema kuwa wamejipanga vizuri katika Matawi ,Kata pamoja na Wilaya hivyo na Mkoa kwa ujumla katika kufanya siasa safi na hawatarajii kuona uwepo wa  uvunjifu wa amani.

Katika Mkutano uliambatana na Wenyeviti wa CCM  wa Wilaya zote za Mkoa wa Iringa na kwa kauli moja   wamesema kuwa pamoja na kuwapo kwa tetesi za mikutano yenye uwazi hawana wasiwasi badala yake wanatarajia mabadiliko makubwa utendaji kazi mzuri katika kipindi hiki.

"Wenyekiti katika wilaya zetu hakuna wasiwasi wala mitetemo tupo vizuri na tupo tayari  kufanya siasa safi licha ya kuwepo kwa baadhi ya maneno yanayotaka kututia wasiwasi na tupo tayari kukudhirishia kuwa tupo vizuri" Wamesema Wenyeviti wa Mkoa wa  Iringa 

Kwa upande wake chifu wa wahehe mkoa wa iringa ADAM SAPI amesema kuwa yupo tayari kushirikiana na vyama vyote vya kisiasa 

Hivyo ni vyema zikafanyika siasa safi na zenye tija kwa wananchi."Kutokana kauri iliyotolewa na Mh Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania kuruhu kufanyika kwa mikutano ya siasa kwa vyama vyote hapa nchini tupo tayali na tutashokana mikono na vyama vyote ili kuleta amani katika nchi yetu"

Na kwaupande wao baadhi ya wananchi wamempongeza MH.Raisi kwa maamuzi hayo kwani wao pia watapata wasaa mzuri wa kuzunguza na viongizi na kutoa kero zao kupitia mikutano hiyo na hivyo kuvitaka vyama hivyo kufanya mikutano yenye amani na masrahi kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Daud Yassin akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan juu ya kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya Siasa nchini baada ya kukaa kwa muda mrefu bila mikutano hiyo,
Chifu wa Kabila la Wahehe Adam Sapi Mkwawa akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na CCM Mkoa wa Iringa wa kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Daud Yassin akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan juu ya kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya Siasa nchini baada ya kukaa kwa muda mrefu bila mikutano hiyo ambapo aliambatana na viongozi wa Mkoa huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...