Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Simba SC imeongeza nguvu kwenye Benchi lake la Ufundi baada ya kumsajili Kocha Msaidizi raia wa Tunisia, Ouanane Sellami (42) kwa mkataba wa miaka miwili, ikiwa ni pendekezo la Kocha Mkuu wa timu hiyo, Roberto Oliviera Robertinho.
Kocha Sellami amesajiliwa na Simba SC kama Kocha Msaidizi akiungana na Kocha Msaidizi mzawa Juma Mgunda. Simba SC wamefanya usajili huo na kuwa na jumla ya Makocha Wasaidizi wawili ili kuongeza nguvu zaidi kwenye Benchi hilo la ufundi katika mashindano mbalimbali.
Sellami ana Shahada ya Uzamili (Masters) ya Elimu ya Viungo ya Michezo kutoka Taasisi ya Superieur Education Sportive Sfax ya nyumbani kwao Tunisia, sanjari na kumiliki Leseni B ya Ukocha ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Pia Kocha huyo aliwahi kuzifundisha timu za Almadina ya Libya mwaka 2022 wakati mwaka mmoja nyuma aliifundisha Gabesien inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Tunisia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...