Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Nyota wa Soka ulimwenguni, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wamekutana uso kwa uso huko Uarabuni katika mchezo wa kirafiki kati ya PSG dhidi ya timu ya Saudi All Stars uliopigwa kwenye dimba la King Fahd International mjini Riyadh nchini Saudi Arabia.

Messi na Ronaldo wamekutana kwenye mtanange huo kwa mara ya kwanza tangu Oktoba 2020, baada ya Juventus kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Barcelona katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA CL) kwenye hatua ya makundi, wakati huo Ronaldo alikuwa Juve na Messi alikuwa Barca.

Katika mchezo huo uliopigwa Januari 19, 2023, uliohitimishwa kwa PSG waliokuwa na Messi kupata ushindi wa mabao 5-4 dhidi ya Saudi All Stars waliokuwa chini ya Nahodha Cristiano Ronaldo ambaye anacheza Al Nassr FC ikiwa ni mara ya kwanza kuanza kucheza timu hiyo tangu ajiunge akitokea Manchester United. 

Mabao ya PSG kwenye mchezo huo yalifungwa na Messi dakika ya 3’ huku bao la pili likifungwa na Mlinzi Marcos Marquinhos dakika ya 43’. PSG walipata ushindi huo kwa mabao mengine ya Sergio Ramos dakika ya 53’, Kylian Mbappé dakika ya 60’ kwa mkwaju wa Penalti na bao la tano lilifungwa na Hugo Ekitiké dakika ya 78’.

Saudi All Stars wakiwa katika ardhi ya nyumbani walipata mabao yao kupitia kwa Nahodha wao, Cristiano Ronaldo kwenye dakika ya 34’ kwa mkwaju wa Penalti na bao la Pili CR7 alifunga tena kwenye dakika ya 45+6’ huku mabao mengine yakifungwa na Jang Hyun-soo dakika ya 56’ na Talisca dakika ya 90+4’.

Paris Saint Germain wapo mjini Riyadh nchini Saudi Arabia kwa mapumziko mafupi wakiwa hapo wamekutana na Kikosi hicho chenye muunganiko wa Wachezaji wanaocheza timu za Al Hilal SFC na Al Nassr FC zote za Saudi Arabia.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...