Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeiagiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), kuhakikisha inazisimamia Taasisi zake kutekeleza majukumu yao katika ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara, madaraja, vivuko, viwanja vya ndege, nyumba na majengo ya Serikali.

Akizungumza jijini Dodoma, katika kikao cha kupokea na kujadili kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo ya Sekta hiyo kwa kipindi cha nusu mwaka cha Julai hadi Desemba iliyosilishwa kwa Kamati hiyo,Mwenyakiti wa Kamti hiyo, Mheshimiwa Selemani Kakoso, amesema kuwa pamoja na mambo mengine amesisisitiza umuhimu wa Sekta hiyo kuongezewa fedha ili kutekeleza na kumaliza miradi hiyo kwa wakati.

“Niipongeze Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa miradi inayoendelea, Tumeshuhudia baadhi ya miradi kukamilika na mengine kuendelea na utekelazaji wake katika mikoa mbalimbali nchini, hivyo naiomba Serikali iendelee kuitengea fedha za kutosha Sekta hii ili iendelee kutekeleza na kukamilisha miradi iliyopanga”, amesema Kakoso.

Aidha, ameiagiza Wizara kuiwezesha Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kuweka mpango madhubuti wa kununua vipuri vya jumla kupitia kwa Makampuni halisi ya magari badala ya kupitia kwa mawakala, hali inayopelekea kwa Wakala kushindwa kufanya matengenezo ya washitiri wake kwa wakati.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Eng. Godfrey Kasekenya, ameaiahidi Kamati hiyo kuendelea kutekeleza miradi yote kwa ufanisi kwa kuzingatia vipaumbele vilivyoweka pamoja na Ilani ya CCM ya Mwaka 2020.

Kasekenya, ameongeza kuwa Wizara (Ujenzi) kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango itahakikisha kuwa fedha za Makandarasi wanaojenga miundombinu mbalimbali inayotekelzwa na kusimamiwa na Sekta hiyo nchini zinalipwa kwa wakati.

Naye, Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Gairo, Mheshimiwa Ahmed Shabiby, ameupongeza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kujenga na kukarabati barabara nchini ambapo ametolea mfano wa barabara ya Morogoro – Dar eneo la Gairo lililokarabatiwa hivi karibuni.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Godfrey Kasekenya, akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Sekta ya Ujenzi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Selemani Kakoso, akisisitiza  jambo kwa viongozi na watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) (hawapo pichani), mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea kwa mwaka wa fedha 2022/23, jijini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Viongozi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), wakifatilia kwa makini taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Godfrey Kasekenya, wakati akiwasilisha kwa Kamati hiyo, jijini Dodoma.

 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambaye ni Mbunge Jimbo la Same Mheshimiwa Anne Kilango, akichangia hoja wakati wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) ikiwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa Kamati hiyo, jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...