MWENYEKITI wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula leo Januari 19, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo Mhe. OM Birla, Spika wa Bunge La India.
Bi. Ngalula amemshukuru Mhe. Birla kwa niaba ya sekta Binafsi kwa kutenga muda wake kuitembelea Tanzania kwani inaonyesha mahusiano mazuri ya diplomasia na uchumi kati ya nchi hizi mbili.
Biashara kati ya Tanzania na India inatarajiwa kufika $6B mwaka 2023. Hii inatokana na kufunguliwa kwa masoko ya bidhaaa za kilimo ikiwepo Maparachichi na nafaka mbalimbali. “ Kwa sasa Tanzania inanunua bidhaa zaidi ya tunavyouza kwenda India, ila tunawaalika wafanyabiashara kutoka India kuwekeza kwenye viwanda vitakavyoongeza thamani ili kuongeza biashara kupunguza tofauti hii.
Alisema Ngalula “Na pia kuendelea kufungua masoko ya bidhaa za Tanzania kwenda India. “ India ndio soko kubwa la bidhaa za Tanzania.
Kwa upande wake Mhe. Spika, alielezea umuhimu wa kuendelea kushirikiana kibiashara kwenye Sekta za Kilimo, Afya, Elimu, teknohama, viwanda, industrial parks.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula akizungumza wakati alipokutana na Spika wa Bunge La India, OM Birla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...