Na Pamela Mollel,Serengeti
Spika wa Bunge la India Mh.Om Birla ameipokeza Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania kwa kuwa na idadi kubwa ya wanyama wakubwa na rahisi kuonekana ndani hifadhi hiyo
Pia ametaja sababu moja wapo ya yeye kuja Tanzania katika hifadhi hiyo ni ile Filamu ya "The Royal Tour" iliyolenga kuonesha vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika Hifadhi zetu hapa Tanzania, ambapo mwigizaji Mkuu alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufanya utalii katika hifadhi hiyo yenye umaarufu mkubwa Duniani alisema kuwa yeye pamoja na timu yake kutoka India wamefurahi sana kuwepo ndani ya Serengeti na wameweza kujionea vivutio mbalimbali kwa ukaribu zaidi
Spika Birla alisema kuwa anaipongeza Tanzania kwa kuwa na vivutio vingi lakini pia Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutangaza utalii wa Tanzania kupitia Filamu ya The Royal Tour
"Royal Tour imenifanya nitamani sanaa kuja katika hifadhi hii ya Serengeti hakika sehemu hii ni nzurii sanaaa kwa kufanya utalii"alisema Spika Birla
Aliongeza kuwa yeye pamoja na timu yake kutoka India wameridhishwa hivyo kuhaidi kuwa mabalozi wazuri wa kutangaza Serengeti katika nchi ya India
"Tukiwa hapa Serengeti tumejionea wanyama wengi sanaaa wakiwemo Simba ,Twiga,Faru,nyumbu na wengine wengi"alisema Spika Birla
Naye Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama ya Bunge Vita Rashid kawawa alisema Spika wa India alipewa mwaliko na Spika wa bunge la Tanzania kama Diplomasia ya kibunge baina ya Tanzania na India
"Leo wameweza kupata picha kuwa Serengeti ni mahali pakuja na kuweza kuonana wanyama wakubwa tena kirahisi zaidi na wakitoka hapa wataweza kututangazia hifadhi na kupitia fursa hiyo tutapata watalii wengi kutoka India"alisema Kawawa
Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Uhifadhi Herman Batiho anayesimamia Uhifadhi na maendeleo ya Biashara alisema wao kama shirika la hifadhi za Taifa Tanapa wamefarijika kupata ugeni huo wenye jumla ya watu 12 wakiongozwa na Spika wa Bunge la India
Alisema kuwa wanatarajia kupata idadi kubwa ya watali kutoka India kuja Tanzania kufanya utalii kutoka na Spika huyo pamoja na wabunge walioambatana nao kuhaidi kuwa mabalozi wazuri wa kutangaza hifadhi ya Taifa Serengeti
"Taifa la India linasifika kwa kuwa na watu wengi zaidi hivyo tunategemea kupata watalii wengi na ugeni huu umefurahi sana kuwepo katika hifadhi hii"alisema Batiho.
Kushoto ni Naibu Kamishna wa uhifadhi Herman Batiho anayesimamia uhifadhi na maendeleo ya biashara akisalimiana na Spika wa bunge la India Mh.Om BirlaSpika wa bunge la India Mh. Om Birla akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti pamoja na timu ya wabunge kutoka nchi hiyo
Kushoto Prosper Minja,Afisa Habari Mwandamizi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ni Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje,ulinzi na usalama ya Bunge Vita Rashid Kawawa,kulia ni Mhifadhi kutoka Shirika la hifadhi za Taifa Tanapa Mohammed Kiganja wakiteta jambo ndani ya hifadhi ya Serengeti
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...