Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike (kulia) akielezea huduma zinazotolewa na Jeshi la Uhamiaji wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga. Wa tatu kushoto ni Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude, wa pili kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma wakiwa katika banda la Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga limeshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa elimu juu ya huduma wanazotoa ikiwemo Utoaji Pasipoti, Vibali vya Ukaazi, Vibali vya kuingia nchini (Visa),kudhibiti uhamiaji haramu, kuendesha kesi za uhamiaji haramu pamoja na kupokea maombi ya uraia.

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Mkoani Shinyanga yamezinduliwa rasmi leo Jumapili Januari 22, 2023 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria mwaka 2023 iliyoanza leo nchini na kutarajiwa kuhitimishwa Februari 1,2023 yanayoongozwa na kauli inayosema, “Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu wajibu wa mahakama na wadau”.

Akizungumza wakati wa Maadhimisho hayo, Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike amesema wanatumia fursa ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria kutoa elimu kwa jamii kuhusu huduma zinazotolewa Idara ya Uhamiaji ambazo ni pamoja na kukagua Fomu za maombi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) sambamba na huduma ya uendeshaji wa kesi zinazohusu wahamiaji haramu na kupokea maombi ya uraia wa Tanzania.

Angumbwike amezitaja huduma zingine wanazotoa kuwa ni Utoaji wa Hati ya Kusafiria (Pasipoti), huduma ya vibali vya ukaazi, vibali vya kuingia nchini (Visa) na huduma ya kudhibiti wahamiaji haramu.

Angumbwike amesema pia Uhamiaji inatoa Huduma kwa njia ya Mtandao (Tanzania E-Immigration Online Portalhivyo kuwahamasisha wananchi kutumia fursa ya Mtandao kupata huduma zinazotolewa Uhamiaji.

"Mfumo wa Passport kwa njia ya mtandao ni huduma mpya inayomuwezesha muombaji kujaza Fomu ya Maombi ya Pasipoti kwa njia ya Kielektroniki akiwa mahali popote. Baada ya kujaza fomu hiyo, atatakiwa kuichapisha (Print) na kuiwasilisha pamoja na vielelezo vingine katika Ofisi ya Uhamiaji iliyo karibu naye kwa ajili ya kushughulikiwa maombi yake ya Pasipoti",amesema Angumbwike.

Akizungumza wakati akifungua maadhimisho hayo, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga watumie fursa ya maadhimisho hayo ya wiki ya Sheria kupata elimu na msaada wa kisheria bure na kupata ufumbuzi wa matatizo yao.
Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike (kulia) akielezea huduma zinazotolewa na Jeshi la Uhamiaji wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga. Wa tatu kushoto ni Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude, wa pili kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma wakiwa katika banda la Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga.
Tembelea Tovuti ya Uhamiaji bofya hapa 👉https://immigration.go.tz/
Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike (kulia) akielezea huduma zinazotolewa na  Jeshi la Uhamiaji wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga. 

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati akizindua Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati akizindua Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023

Maafisa wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu na meza kuu wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023.
Maafisa mbalimbali wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria Mkoa wa Shinyanga leo Jumapili Januari 22,2023.

Picha zote na Kadama  Malunde - Malunde 1 blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...