Wakuu wa Taasisi za Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo tarehe 6 Januari, 2023 wamekutana kwenye Tamasha la 9 la Biashara Zanzibar na kufanyanya mazungumzo yaliolenga kuendeleza ushirikiano katika kutatua changamoto na kuboresha huduma kwa Wafanyabiashara wa pande zote mbili.
Akizungumza katika Mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Rashid A. Salim amesema kunachangamoto ambazo zinaweza kutatuliwa endapo Taasisi hizo zitashirikiana katika kupeana taarifa , kufanya mafunzo ya pamoja, kushiriki mikutano na kushirikiana katika kuaandaa miradi.
Ndugu Salim ameongeza kuwa Mkutano huo ni hatua muhimu katika kudumisha Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana katika kuhahikisha Taasisi hizo zinawawezesha Wafanyabiashara Nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa Khamis amesema Mkutano huo umewaleta pamoja Wakuu wa Taasisi na kujadiliana mada zilizolenga kutatua changamoto katika usajili wa Biashara na leseni, Ushindani na halali, Viwango na Vipimo, Viwanda na Biashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...